Kamanda Lazaro Mambosasa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa
amesema Jeshi la Polisi linamshikilia kwa mahojiano mwandishi wa... habari
Erick Kabendera aliyekamatwa Julai 29, 2019 nyumbani kwake maeneo ya
Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Kamanda Mambosasa amesema, mtuhumiwa huyo alikamtwa baada ya kukataa
wito wa polisi ambapo awali aliandikiwa barua ya wito kwa ajili ya
mahojiano, lakini alikaidi kutii wito huo na kusema kwamba, jeshi la
polisi linapomuita mtu kwa hiari na akaacha kutii wito huo, hutumia
mbinu ya kumlazimisha atii.
''Baada ya kukamatwa mwandishi huyo, tulisikia taarifa mbalimbali kutoka
kwa kada mbalimbali kwenye jamii wakiendelea kusema mwandishi huyo
alitekwa niseme kuwa, mwandishi huyo hakutekwa aliitwa, lakini kwa jeuri
alikaidi kutii wito huo, sababu pia ya kuitwa ni kuhusiana na utata wa
uraia wake, Jeshi linaendelea na upelelezi kwa kushirikiana na maafisa
wa uhamiaji'', amesema SACP Mambosasa.
Aidha Kamanda Mambosasa ameongeza kuwa, baada ya upelelezi kukamilika
jeshi hilo litahakikisha kosa analotuhumiwa nalo mwandishi huyo,
linawekwa mezani ili na yeye aweze kuhakikishia kama ni mtanzania kwa
kutoa vielelezo vinavyothibisha uraia wake.
No comments :
Post a Comment