Monday, July 1, 2019

Picha : BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO (AQRB) YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI


Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Arch. Dkt Ludigija Bulamile akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishishi wa habari Jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na bodi hiyo kuhusu kuacha kuichanganya taaluma yao na ile ya wahandisi badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu
hao wanapofanya ujenzi. Picha zote na Philemon Solomon
Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Arch.Albert Munuo, akisoma taarifa kuhusu majukumu ya bodi hiyo (kulia) Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Ludigija Bulamile.
Afisa Mkuu wa Sheria Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Ibrahim Mohamed akielezea makosa mbali mbali ya kisheria yanayofanywa yakiwemo yale ya uuzwaji wa ramani hadharani pasipo kufuata taratibu. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Arch . Dkt Ludigija Bulamile akipitia taarifa mbali mbali za bodi hiyo.
Watumishi wa bodi hiyo wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishishi wa habari yaliyoandaliwa na bodi hiyo kuhusu kuacha kuichanganya taaluma yao na ile ya wahandisi badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu hao wanapofanya ujenzi.
Afisa Mdhibiti Mwandamizi wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Mlezi Makuka (kushoto aliyesimama) akichangia mada yake wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishishi wa habari yaliyoandaliwa na bodi hiyo kuhusu kuacha kuichanganya taaluma yao na ile ya wahandisi badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu hao wanapofanya ujenzi.
Arch. Mbaraka Igangula akichangia mada.
QS.Mashaka Bundara akisisitiza jambo.
Arch.Joseph Ringo akichangia mada wakati wa mafunzo hayo.
Waandishi wa Habari wakichangia mada mbali mbali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) kuacha kuichanganya taaluma yao na ile ya wahandisi badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu hao wanapofanya ujenzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Dkt. Ludigija Bulamile akijibu maswali.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Dkt. Ludigija Bulamile, Kaimu Msajili Albert Munuo pamoja na waandishi wa habari na wajumbe wa bodi hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) 
 ****
BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) imewataka wanahabari nchini kuacha kuichanganya taaluma yao na ile ya wahandisi badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu hao wanapofanya ujenzi.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo ya
kuwajengea uwezo waandishishi wa habari yaliyoandaliwa na menejimenti ya bodi hiyo mwishoni mwa wiki Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa AQRB Dkt. Ludigija Bulamile alisema lengo ni kuwaelimisha waandishi shughuli na majukumu yake katika sekta ya ujenzi ili waweze kuuelimisha umma wa
watanzania faida na hasara za kutowatumia wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi wanapofanya ujenzi wowote. 
Alisema kumekuwa na mkanganyiko wa utoaji taarifa
unaofanywa na waandishi wakati wanaripoti masuala yanayohusu taaluma hizo hivyo ili kuondoa mkanganyiko huo wanahabari wana kila sababu ya kuyatumia mafunzo haya kwa kuwaelimisha wengine kuzitumia kalamu zao
kuuelimisha umma tofauti za taaluma hizo.
'Elilimisheni jamii umuhimu wa kuwatumia wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi katika ujenzi ili waweze kupata makazi bora, ambayo pia yatawapa nafuu kwenye gharama za ujenzi kulingana na matakwa,'alisema Bulamile. 
Aliongeza kufafanua zaidi sababu za wahandisi kufahamika zaidi na umma kuliko wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi pamoja na kufanya kazi zinazoshabihiana kuwa ni pamoja na taaluma hiyo kuchelewa kuingia  nchini. 
"Mpaka sasa nchi nzima ina wataalamu wa taaluma hii wasiozidi 1,500 hili bado ni tatizo kulingana na idadi ya
watu na mahitaji yake," alisema Dkt. Bulamile na kuongeza bodi imeendelea kuongea na baadhi ya vyuo vikuu vilivyopo nchini vione umuhimu wa kufundisha taaluma hii ili kuongeza idadi ya wataalamu watakaowezesha kuibadili
sura ya nchi hapo baadae katika sekta ya ujenzi kwa kubuni majengo ya kisasa yanayoendana na wakati.
Kwa upande wake Kaimu Msajili wa bodi Mkadiriaji Majenzi
Albert Munuo alisema kuwa,pamoja na kusajili wataalamu wa fani hiyo na makampuni pia wanamajukumu ya kukagua miradi ya ujenzi inayoendelea ili kuona kama wataalamu wamehusika.
" Tumekuwa tukikagua ujenzi wa miradi mbalimbali 
mikubwa inayoendelea na kwamba kwa sasa tunajipanga kuutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR ili kujionea ni kwa namna gani Wabunifu Majengo na
Wakadiriaji Majenzi wameshiriki ,'alisema Munuo
Aliongeza kuwa AQRB ni taasisi ya serikali iliyopo chini ya
Wizara ya Ujenzi na kwamba mpaka sasa ina ofisi katika kanda tano ikiwepo Kanda ya Mashariki, kanda ya ziwa, kanda ya kaskazini ,nyanda za juu kusini na kanda
ya kati. 
Mafunzo hayo pamoja na kuhudhuriwa na baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali zikiwepo televisheni, redio na magazeti pia wataalamu wengine wa ujenzi kutoka AQRB akiwepo mwanasheria wao alishiriki na kusema yapo makosa mbali mbali ya kisheria yamekuwa yakifanywa ikiwepo lile la uuzwaji wa ramani hadharani pasipo kufuata taratibu. 
Hata hivyo wataalamu hao waliongeza kutolea mfano kwa kusema asilimia 90 ya nyumba zilizojengwa Dar es salaam zimejengwa bila vibali na kusababisha hasara kwa jamii pale ambapo eneo hilo linapokuja kubainika kuwa si mahali sahihi kwa ujenzi wa makazi na kulazimika kubomolewa.

No comments :

Post a Comment