Friday, July 26, 2019

MENEJA MAWASILIANO WA SHIRIKA LA AGPAHI, BI AGNES KABIGI AFARIKI GHAFLA HUKO KAHAMA SHINYANGA


R.I.P AGNES KABIGI 
Meneja Mawasiliano wa asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Bi. Agnes Kabigi amefariki dunia leo Ijumaa Julai 26,2019.
Taarifa za awali zinasema Agnes Kabigi ambaye ni mwandishi wa habari wa... muda mrefu aliyetumikia vyombo mbalimbali vya habari kuamnzia miaka ya 90 amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla wakati akitekeleza majukumu yake wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Taarifa za kifo cha Agnes Kabigi aliyewahi kuwa mwandishi wa gazeti la Nipashe katika ngazi mbalimbali zimethibitishwa na Mkurugenzi wa Shirika la AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa.

"Ni kweli ndugu yetu Agnes Kabigi ametutoka,amefariki dunia huko Kahama baada ya kuanguka akiwa kwenye majukumu ya kikazi" - Dkt. Mwakyusa.

No comments :

Post a Comment