
Waziri
wa Mambo ya ndani Ya Nchi Kangi Lugola amemuondoa madarakani Mkuu wa
Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO), Charles Bukombe na
ameagiza achukuliwe hatua kali za kisheria kwa kutokufuata maagizo
anayoyatoa na kuyaita yakisiasa. Na pia ametoa onyo kali kwa Ma-RTO wa
Mkoa wa Morogoro na Mara.
Taarifa
iliyotolewa leo Jumapili Julai 28, 2019 na ofisi ya mawasiliano ya
wizara hiyo imeeleza kuwa licha ya kumuondoa katika nafasi hiyo, Lugola
amemuagiza katibu mkuu wa wizara yake, kumchukulia hatua za kinidhamu
RTO huyo ili iwe fundisho kwa trafiki.
Lugola
amesema amemshuhudia Bukombe katika video inayosambaa mitandaoni
alipokuwa katika mkutano jijini Arusha, akipinga maagizo yake na kuyaita
ya kisiasa na hakuyatekeleza.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara katika mji wa Malinyi mkoani Morogoro leo
Lugola amesema hatoi maagizo ya kisiasa, hutuo yanayomsaidia Rais John
Magufuli katika kazi zake.
No comments :
Post a Comment