
Meneja
wa Bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga, (kushoto) akionyesha kwa
waandishi wa habari simu mpya za Smartphone aina ya TECNO S3 na TECNO
R7, wakati wa uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Saba Saba jijini
Dar es Salaam. (kulia) ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile,
Eric Mkomoya.
Meneja
wa Bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga, (kushoto) akimsikiliza
Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya (kulia) wakati
akionyesha kwa waandishi wa habari simu mpya za Smartphone aina ya TECNO
S3 na TECNO R7, wakati wa uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Saba
Saba jijini Dar es Salaam leo
Meneja wa Bidhaa za intaneti wa Tigo,Mkumbo Myonga, (kushoto)
akimkabidhi zawadi ya simu aina ya TECNO S3 mmoja wa waandishi wa habari
waliojishindia zawadi ya simu wakati wa uzinduzi simu hizo uliofanyika
katika viwanja vya Saba Saba.jijini Dar es Salaam (kulia) ni Meneja
Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya.
Meneja wa Bidhaa za intaneti wa Tigo,Mkumbo Myonga, (kushoto)
akimkabidhi zawadi ya simu aina ya TECNO S3 mmoja wa waandishi wa habari
waliojishindia zawadi ya simu wakati wa uzinduzi simu hizo uliofanyika
katika viwanja vya Saba Saba.jijini Dar es Salaam (kulia) ni Meneja
Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya.
Meneja
wa Bidhaa za interneti wa Tigo, Mkumbo Myonga, (kushoto) akiwa na
waandishi wa habari waliojishindia zawadi ya simu za TECNO s3 na TECNO
S7 wakati wa uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Saba Saba. (kulia)
ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya.
*Kuwezesha mteja kupata... Intaneti bure kwa mwaka mmoja
Kampuni inayoongoza kwa ubunifu wa kidigitali ya Tigo kwa kushirikiana
na kampuni ya kimataifa ya kutengeneza simu za kisasa ya TECNO Mobile
,zimezindua aina mbili mpya ya simu janja za kisasa (smartphones) aina
ya TECNO S3 na TECNO R7, katika soko la Tanzania,ambazo zitapatikana
kwa bei nafuu na kuwawezesha wateja kufurahia matumizi ya Intaneti
kupitia aina za vifurushi watavyochagua kujiunga nayo.
Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika leo katika uwanja wa maonyesho
ya Saba Saba,Meneja wa Bidhaa za Intaneti wa Tigo Tanzania,Mkumbo
Myonga,alisema kuzinduliwa kwa simu mpya kwa ushirikiano na kampuni ya
TECNO Mobile, kwa mara nyingine kunadhihirisha mkakati wa kampuni ya
Tigo katika ubunifu wa kidigitali nchini na kufanikisha kuongeza
watumiaji wa simu janja,watumiaji wa huduma za data na interneti ya
kisasa ya 4G.
“Tunayo furaha kushirikiana na TECNO Mobile leo kuzingua aina mbili za
simu janja za kisasa kwa mwaka huu wa 2019.Simu aina ya TECNO S3 na
TECNO R7 ni simu zinazatikana katika mtandao wa Tigo pekee katika soko
na zinapatikana kwa gharama nafuu ambazo wateja wengi wanamudu
kuzinunua”,alisema Myonga.
Myonga alieleza kuwa Tigo inatoa MWAKA MMOJA WA BURE wa kutumia internet
kwa wateja watakaozinunua ambapo watakaonunua simu aina ya TECNO R7
watapata (GB54) ambazo zinawezesha matumizi ya internet ya 4G na inauzwa
kwa bei ya shilingi 124,900/-.
Kwa wateja watakaonunua simu aina ya TECNO S3,ambayo inawezesha matumizi
ya internet ya 3G,watakuwa na uhuru wa kuchagua ofa wanayotaka, ya
kwanza MWAKA MMOJA WA BURE wa kutumia internet kutokana na kupatiwa GB
48 na gharama ya kununua simu iyo ni shilingi 95,000/-.Ofa ya pili kwa
kunua simu inayouzwa shilingi shilingi 74,900/- na kujipatia internet
yenye GB3 ambayo inawezesha mteja kuitumia miezi mitatu bure.Simu hizi
mpya katika soko la Tanzania zinapatikana katika maduka yote ya Tigo
nchini na zitapatikana katika banda la maonyesho la Tigo lililopo katika
uwanja wa maonyesho ya Saba Saba.
Kwa upande wake,Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric
Mkomoya, alisema kuzinduliwa kwa simu aina ya TECNO S3 na TECNO R7
kupitia mtandao wa Tigo umelenga kuwezesha wananchi wengi kutumia simu
janja na kuweza kufurahia mapinduzi ya ubunifu wa kidigitali ya matumizi
ya simu hizi.
“Simu aina ya TECNO R7 imetangenezwa ikiwa na kioo cha ukubwa wa inchi
5,ina scanner ya kisasa,kamera yenye uwezo wa mega 5 upande wa mbele na
nyuma na flashi inayowezesha kuchua picha kwa kiwango cha ubora wa
juu,imetengenezwa kwa ubunifu wa tekbolojia mbalimbali za kisasa
zinazowezesha matmizi ya internet na kupiga picha.Simu ya aina ya TECNO
S3 imetengenezwa kwa teknolojia za kisasa zinazowezesha matumizi ya
teknolojia ya Android Go OS ,inao ukubwa wa kioo cha mbele cha inchi
4,inawezesha matumizi ya teknolojia za GPS na dual SIM,ambazo
zimeongezwa katika simu za Tecno tolea la sasa hivi,”alisema Mkomoya.
Simu zote za TECNO S3 na TECNO R7 zina waranti ya miezi 13.


No comments :
Post a Comment