Wananchi
wakipata huduma katika banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA
katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani
Lindi.
Wananchi
wakipata huduma katika Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel kwa ajili
ya kusajili kwa alama za vidole katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada
Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani.
Afisa
Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel
Masasi akitoa huduma kwa mwananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada
Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi.
Wananchi
wakipata elimu katika Banda la TCRA katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada
katika enoo la Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi.
Afisa
Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
akizungumza na Wananchi wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi
katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada kuhamasisha wananchi kusajili laini za
simu kwa alama vidoleNA MWANDISHI WETU, KILWA
Wakazi
wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi na viunga vyake
wamejitokeza kwa wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi
la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA) kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu
kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu
kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.
Afisa
Mawasiliano Mwandamizi ya TCRA Mabel Masasi amesema ni fursa kwa
wananchi wa Bukoba kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa
mawasiliano. Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya
kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu
changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.
Masasi
amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe
wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na
huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.
Amesema
kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi
Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa
ya jinai ya matumizi ya simu.
Aidha
amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha
kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia
kitambulisho cha taifa cha NIDA."TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia
wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa
kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema Masasi.














No comments :
Post a Comment