Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizindua rasmi na kutembelea
maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara.
Na Christian Gaya Majira Ijumaa 12. Julai. 2019
Maonesho ya 42
ya Biashara ya Kimataifa, maarufu kama Sabasaba yalifunguliwa rasmi siku ya
Jumanne na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na yanatarajiwa kufikia kilele kesho Julai
13, 2019 katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es
Salaam.
Kauli
mbiu ya mwaka huu ni "Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa maendeleo endelevu
ya
viwanda." Ili kuleta tija kwa nyanja zote wakiwamo wakulima na wazalishaji
wa viwandani. Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania imejipanga kuhakikisha
sekta ya kilimo na viwandani zinabebana kwa kufanya shughuli zake kwa
kutegemeana ili kuleta tija kwa kila upande.
Sekta ya kilimo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa
uchumi wa Tanzania, Sekta
inatoa ajira kwa asilimia 65.5, huchangia asilimia 29.1ya pato la Taifa, asilimia 30 ya fedha za kigeni, asilimia 65 ya malighafi za viwanda, Asilimia 100 ya chakula (Nchi inajitosheleza
na tuna ziada ya kuuza nje.
Nafasi ya kilimo katika viwanda ni kwamba viwanda
vingi vinategemea kilimo, na asilimia
65 ya malighafi za viwanda zinatoka sekta ya kilimo yakiwemo mazao, mifugo na
uvuvi. Kilimo
kisipoimarika viwanda vitakosa malighafi bora na za kutosha wingi na ubora wa mazao ya kilimo ndivyo vina
unatuhakikishia na kushawishi watu kuwekeza katika viwanda. Kuimarika kwa viwanda ni fursa ya masoko ya
mazao,mifugo na uvuvi, hivyo
kuimarisha kilimo ni kuimarisha viwanda, mapato na ajira kwa watanzania na
uchumi kwa ujumla na kuongezeka kwa idadi kubwa ya wanachama watakaochangia
mifuko ya hifadhi ya jamii na hatimaye kuwa na afya nzuri kwa ajili ya faida ya
wanachama, wastaafu na wafamilia zao.
Na ndiyo maana hata mfuko wa taifa wa hifadhi wa NSSF umeshirika
kwa ajili ya kutoa elimu kwa wafanyakazi wafanyakazi
kutoka sekta binafsi na sekta isiyo kuwa
rasmi.
Asilimia 90 ya ardhi ya Tanzania hulimwa na wakulima
wadogo ambao wote wako karibu kwenye sekta isiyo rasmi ambayo ipo chini ya
mfuko wa NSSF
Kulingana na sensa ya watu
iliyofanyika kitaifa mwaka 2012 Tanzania inakadiriwa kuwa na watu milioni 45,
ambapo nguvukazi ya watu wa umri kati ya miaka 15-60 ni milioni 22.7, na kati
yao milioni 1.2 tu ndio walio katika ajira rasmi ambapo watu milioni 1.1 tu
ndio wanahudumiwa na hifadhi ya jamii.
Hii ina maana kuwa watu
milioni 21.6 ndio walioko katika ajira binafsi na hawafikiwi na mifuko ya
hifadhi ya jamii. Pamoja na kwamba
sekta isiyo kuwa rasmi ndiyo yenye ajira kubwa kwa watanzania lakini sehemu
kuwa ya wafanyakazi wake hawana elementi yeyote ya aina ya kinga ya hifadhi ya
jamii ingawa hata ufanisi wa kazi zao uko chini sana.
Hivyo
inaonesha kwamba waathirika zaidi wako vijijini ambako asilimia kubwa ya wakazi
wake hawana kabisa huduma za afya kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii.
Uzoefu
huu unashawishi kuwa mfuko wa NSSF sasa utazame katika sekta ya kilimo. Kilimo
ndio sekta mama ya uchumi wetu na inaajiri zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wetu, ingawa ukuaji wake ni asilimia 4.4 ambayo ni chini ya kiwango
kinachotakiwa cha asilimia 6 kwa
mwaka kutokana na kukosa uwekezaji wa kutosha.
Ni
juu ya NSSF kushirikiana na taasisi husika kuhakikisha ya kuwa wakulima wadogo wote wanapitia katika ushirika wao ili iwe rahisi
kuwahamasishwa kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii na kwa mtindo huu itakuwa rahisi hata kushiriki
katika kuongeza thamani mazao yao kabla ya kuuza na kuwawezesha kuwa na nafasi
kubwa ya kulipa michango ya hifadhi ya jamii kila wakati inapotakiwa kupelekwa.
Ili
jambo hili liwe endelevu na kuwezesha mfuko wa NSSF kuwapata wanachama wengi
zaidi watatakiwa kuwa na mijadala ya mara kwa
mara kati ya vyama vya wakulima na serikali pamoja. Wakulima wanatakiwa wasaidiwe ili kuongeza
tija na uzalishaji na ili nchi ipate malighafi ya kutosha yaani kuwe na mifumo
mizuri ya upatikanaji wa pembejeo.
Na pia kuwe na mifumo imara ya
masoko kwa mazao hata ya chakula ili kuhamasisha uzalishaji na kuepukana na
zuia la uuzaji nje ya nchi
Viwanda vya usindikaji
visogezwe kwa wakulima ili washiriki kuongeza thamani. Benki ya kilimo na benki
zingine kama vile ya Azania Benki zinatakiwa ziwakopeshe wakulima kwa riba na
masharti nafuu.
Uwekezaji mkubwa unahitajika katika miundombinu kilimo
kama vile umwagiliaji, mifugo, uvuvi masoko na barabara za vijijini. Vijana wapatiwe upendeleo maalumu ili washiriki
kikamilifu katika kilimo. Vivutio
kwa wawekezaji wa ndani na nje kama vile
kuondoa kodi katika ardhi kutavutia watu wengi kurasimisha ardhi.
Ili kuufanya mfuko huu uwe
na afya zaidi na idadi kubwa ya wakulima wadogo wawe na kinga ya hifadhi ya
jamii, hivyo ni vema mazungumzo kati ya serikali na sekta binafsi yakaboreshwa
ili serikali ipate kujua mahitaji ya sekta binafsi na sekta isiyo rasmi katika
kufanikisha mpango huu.
Chukulia
ya kuwa idadi kubwa wanaohudhuria na kushiriki maonesho haya ya 43 wengi ni wa usindikaji wa mazao ya kilimo kwa
maendeleo endelevu ya viwanda kwa maana kweli wanaendana na kauli mbiu ya mwaka
huu.
Ambapo
idadi kubwa ya wasindikikaji wote hawana hata kinga ya hifadhi ya jamii na wote
wanaangukia kwenye mfuko wa NSSF unaoshughulika na sekta binafsi na sekta isiyo
rasmi kisheria. Hiyo fursa kubwa kwa mfuko wa NSSF kuitumia ipasavyo.
Hii ina maana kwamba matumizi ya fedha za umma katika kupanua wigo wa
huduma hii lazima yaongezwe ili idadi ya wanufaika iongezeke hasa kutoka katika
hizi yaani sekta isiyo rasmi na sekta binafsi ambako kuna uwekezaji mdogo zaidi
kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
Washiriki wa maonesho na
wananchi wote kwa ujumla mnaotembelea maonesho haya tembeleeni banda la NSSF
ili mpate kujibiwa maswali yote mliyo nayo na ili kutatuliwa kero zanu papo kwa
papo. Wanachama na wananchi mnahamasishwa
kutembela banda hilo ili kupata huduma na taarifa mbalimbali kuhusu shughuli za
mfuko wa NSSF
Huduma zitolewazo na NSSF kwenye banda hilo namba 13 ambalo pia
linatumiwa na Mfuko wa PSSSF, ni pamoja na taarifa za Uhakiki wa wastaafu,
taarifa za pensheni ya uzee, taarifa za mafao ya kukosa ajira, taarifa za Mafao
ya uzazi, taarifa za dhamana ya mikopo ya nyumba na na taarifa za uwekezaji
No comments :
Post a Comment