SHEIKH Khamis Gharib Khamis akiongosa Sala ya Eid Fitry katika viwanja vya Maisara Suleiman leo,(Picha na Ikulu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Msikiti wa Anwari
uliopo Msasani jijini Dar es salaam, Sheikh Alhaji Suleiman Mohammed
wakati alipowasili msikitini hapo kuswali Swala ya Eid El Fitr, Juni 5,
2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika Swala ya Eid El Fitr kwenye
Msikiti wa Anwari, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 5, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika Swala ya Eid El Fitr kwenye
Msikiti wa Anwari, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 5, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika Swala ya Eid El Fitr kwenye
Msikiti wa Anwari, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 5, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Swala ya Eid El Fitr kwenye
Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 5, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Swala ya Eid El Fitr kwenye
Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 5, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
TUTUMIE SIKU YA EID KWA KUTENDA MEMA-MAJALIWA
NA OWM
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amewataka waislamu wote nchini watumie siku kuu
ya Eid el Fitr kwa kutenda matendo mema pamoja na kuwakumbuka yatima na
wajane.
“Leo
ni siku kubwa na muhimu waislamu wanahitimisha mfungo wa Mwezi Mtukufu
wa Ramadhani na kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, hivyo tuendeleze
matendo mema.”
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Juni 5, 2019) wakati aliposhiriki
swala ya Eid El Fitr katika msikiti wa Anwar uliopo Msasani jinini Dar
es Salaam.
Waziri
Mkuu amesema wakati huu ni mzuri kwa kuimarisha mshikamano miongoni
mwenu na madhehebu mengine, hivyo hakikisheni mnayaendeleza mambo mema
yote.
“Tumeona
utulivu uliojitokeza katika mwezi mtukufu, na jambo hili limesisitizwa
na viongozi wa dini. Tuendelee kuwa wamoja, tuimarishe mshikamano na
tuvumiliane.”
Pia,
Waziri Mkuu amewakumbusha wazazi na walezi kuwaongoza watoto kwa kuwapa
mafundisho ya dini yatakayowawezesha kumjua Mwenyezi Mungu na kuwa raia
wema.
Awali,
Imamu wa msikiti huo, Sheikh Mhina alisema waislamu wanatakiwa kuitumia
siku ya leo kwa kuhamasisha Amani pamoja na kuwasaidia watu wasiokuwa
na uwezo.
Pia
amewasisitiza wayaendeleze mema yote waliyoyafanya katika kipindi cha
mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu na kuwajali
wazazi wao.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Swala ya Eid El Fitr kwenye
Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam, Juni 5, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waumini wa Dini ya Kiislamu
baada ya kushiriki katika Swala ya Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwar,
Msasani jijini Dar es salaam, Juni 5, 2019. Kulia ni Mwenyuekiti wa
Msikiti huo, Sheikh Alhaji, Suleiman Mohammed. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watoto baada ya kushiriki Ibada
ya Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam
Juni 5, 2019., (Picha na ofis ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Bw. Mohammed Iqbal Noray baada ya
kushiriki Swala ya Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini
Dar es salaam, Juni 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watoto baada ya kushiriki Ibada ya
Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam Juni
5, 2019., (Picha na ofis ya Waziri Mkuu)| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watoto baada ya kushiriki Ibada ya Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam Juni 5, 2019., (Picha na ofis ya Waziri Mkuu) |
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Alhajj Ali
Mohamerd Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.
Balozi Seif Ali Iddi alipowasili katika viwanja vya Maisara Suleiman
kuhudhuria Ibada ya Sala ya Eid Fitry leo,5-6-2019.(Picha na Ikulu)
NA IKULU, ZANZIBAR
NA IKULU, ZANZIBAR
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed
Shein amewanasihi wananchi kutii sheria za nchi ili wageni
wanaoitembelea Zanzibar nao waweze kuiga mfano wao na hatimae waendelee
kuishi kwa hali ya salama na amani.
Alhaj
Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa katika Baraza
la Idd El Fitri kwenye ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil, Kikwajuni
mjini Zanzibar hafla ambayo imehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa
vyama vya siasa na Serikali akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Idd, Mabalozi Wadogo waliopo Zanzibar na wananchi.
Katika
hafla hiyo, ambapo Mama Mwanamwema Shein nae alihudhuria, Dk. Shein
alieleza kuwa kuwepo kwa amani na utulivu nchini kumzidisha kupiga hatua
za ufanisi za utekelezaji wa mipango mikuu ya maendeleo ambayo ni MKUZA
III, Dira ya Maenedeleo ya 2020, Mpango wa Dunia wa Maendeleo Endelevu
na Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2015-2020.
Rais
Dk. Shein alisema kuwa nchi inayothamini na kufuata misingi ya utawala
bora watu wake huwa na uvumilivu maalum wa kuishi pamoja katika jamii
yenye watu wenye imani tafauti za kidini na kiutamaduni.
Aliongeza
kuwa watu wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla wamekuwa ni kigezo
kizuri miongoni mwa nchi kadhaa duniani katika kuuendeleza ustaarabu huo
wa uvumilivu tangu hapo kale na dahari.
“Kwa
hakika uvumilivu ni miongoni mwa sababu zinazotuepusha na migogoro ya
wenyewe kwa wenyewe nchini. Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa tunu
hii, tutahakikisha kwamba tunailinda amani na usalama nchini mwetu kwa
kila hali”alisema Alhaj Dk. Shein.
Aidha,
alisisitiza kuwa wananchi wa Zanzibar wanawajibu wa kumshukuru Mwenyezi
Mungu kwa kuwajaalia kuwa na uchumi unaokuwa mwaka hadi mwaka ambapo
katika mwaka wa fedha 2018 uchumi ulikuwa kwa asilimia 7.1 kutoka 7.0 na
mfumko wa bei uliendelea kushuka kutoka kasi ya asilimia 5.6 mwaka 2017
hadi kufikia asilimia 3.9 mwaka 2018.
Alieleza
kuwa katika kuimariska kwa uchumi makusanyo ya mapato yameongezeka na
kufikia TZS bilioni 6668.70 mwaka 2017/2018 kutoka TZS bilioni 181.48
mwaka 2010/2011 ambayo ni sawa na ongezeko la mara 3.7.
Dk.
Shein alisema kuwa pato la mtu binafsi ambalo lilikuwa TZS 942,000
mwaka 2010, limeongezeka na kufikia TZS 2,323,00O mwaka 2018 ikiwa ni
sawa na ongezeko la asilimia 146.7.
Hivyo,
alisema kuwa makusanyo na utekelezaji wa mipango ya maendeleo inaleta
matarajio ya kukua kwa uchumi kufikia asilimia 7.8 katika mwaka wa fedha
wa 2019/2020 na hapana shaka kwamba Zanzibar itafikia nchi yenye uchumi
wa kati ifikapo mwaka 2020 kama ilivyolengwa katika Dira ya Maendeleo
ya Zanzibar ya 2020.
Pamoja
na hayo, Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa Serikali haina uwezo wa kumpa
kila mtu mmoja pesa za matumizi katika kuendeleshea maisha yake ila
humlipa kupitia huduma mbali mbali zinazotoa kwa wananchi.
Kwa
hivyo, kila kiongozi kwa nafasi aliyo nayo itamlazimu asimamie suala la
ulipaji kodi pamoja na utoaji wa risiti na kuwataka wananchi kuendelea
kushajiishana juu ya utoaji na uchukuaji wa risiti ili kuhakikisha
kwamba kila senti inayolipaswa kukusanywa na Serikali inakusanywa.
Alitoa
wito kwa wafanyabiashara watambue umuhimu wa kutoa risiti zilizohalali
katika biashara zao na kulipa kodi kwa mujibu wa sheria kwani ni dhahiri
kuwa sehemu kubwa ya mapato ya nchi yanatokana na kodi.
Dk.
Shein alisema kuwa Serikali imeridhika na kiwango cha uwajibikaji
kilichooneshwa na Wizara zote na Taasisi zake katika kutumia fedha
zilizoidhinishwa na Wizara zote na Taasisi zake katika kutumia fedha
zilizoidhinishwa na Baraza la Wawakilishi kwa mujibu wa sheria na
taratibu za matumizi zilizopo.
Kwa
mnasaba huo, Rais Dk. Shein ametoa pongezi kwa Mawaziri, Manaibu
Mawaziri, Watendaji na Watumishi wote wa Serikali na Taasisi zake kwa
mafanikio hayo na ufanisi unaoendelea kupatikana katika kukuza uchumi,
kuimarisha huduma za wananchi na kuwapatia huduma mbali mbali kwa
ufanisi.
Alhaj
Dk. Shein aliwaeleza wananchi kuwa mafanikio yameanza kupatikana katika
kuimarisha huduma za sekta zilizogatuliwa katika kuwatumikia wananchi
na changamoto zinazojitokeza katika kipindi hichi cha mpito zikiwemo
uhaba wa baadhi ya wataalamu, ufinyu wa nafasi za ofisi za kufanyia
kazi, nyenzo za kufanyia kazi na mambo mengineyo zisiwe sababu ya kuona
mfumo wa ugatuzi haufai.
Alisema
kuwa Serikali inaendelea na jitihada zake za kuifanyia kazi changamoto
inayoendelea kuwakabili wananchi ya uharibifu wa miundombinu ya barabara
pamoja na madaraja katika mzimu wa mvua.
Dk.
Shein alitoa pongezi kwa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
kwa kutekeleza agizo alilowapa la kulitafutia ufumbuzi wa kudumu tatizo
la maji la Kibonde Mzungu kwa kujenga daraja la kisasa na kuiagiza
kuendelea na kazi ya kuiunganisha barabara ya Fuoni kutoka kwenye kituo
cha Polisi hadi Kibonde Mzungu huku akitoa pole kwa wananchi wote
waliopata athari kutokana na mvua za masika.
Alisema
kuwa katika jitihada za kuimarisha miundombinu ya barabara, Serikali
imenunua mtambo wa lami wa kisasa pamoja na kuagiza zana na vifaa vya
kisasa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara pamoja
na ukarabati wa baadhi ya barabara za Unguja na Pemba vyote vikiwa na
thamani ya TZS Bilioni 14.8.
Sambamba
na hayo, alitoa shukurani kwa uongozi na wafanyakazi wa Wizara ya
Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kwa
kuwapatia huduma ya maji wananchi ambao huduma hiyo hawaipati vyema
katika maeneo yao.
Alitoa
shukurani kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa ajili ya kusimamia
ulinzi wa nchi katika maeneo yote, kusimamia hali ya usalama wa wananchi
na kukabiliana na madereza wanaovunja sheria za usalama barabarani.
Alhaj
Dk. Shein aliwaombea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwapa afya njema,
Waislamu wanaokwenda kutekeleza Ibada ya Hijja huko Saudi Arabia mwaka
huu ili waweze kuitekeleza vyema ibada hiyo.
Alisisitiza
kuwa ili ufanisi upatikane katika maendeleo ya jamii ni vyema wananchi
wakaendelea na mwenendo mzuri wa kutafuta radhi za Allah hata katika
miezi mingine baada ya kumaliza kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Aliwasihi
Mashekhe na Walimu waendelee kutoa mawaidha juu ya umuhimu wa
kuyaheshimu maamrisho ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata mwenendo wa maadili
mema na kubainisha madhara ya kuhalifu maarisho ya Mola.
Akitoa
tafsiri na maelezo mafupi ya Aya za Qur-an tukufu Surat Muuminuna
kuanzia Aya ya 1 hadi ya 11, Sheikh Abdallah Hamid Suleiman kutoka Chuo
Cha Kiislamu alisisitiza haja ya umoja na mshikamano kwa waumini wa dini
ya Kiislamu na wananchi wote sambamba na kukemea vitendo viovu na
kufanya mambo mema na kuyafuata maarisho ya Mwenyezi Mungu.
Mapema,
Rais Dk. Shein aliungana na wananchi pamoja na viongozi mbali mbali wa
Dini na Serikali katika sala ya Idd El Fitri iliyosaliwa katika viwanja
vya Maisara, mjini Zanzibar ambapo katika hotuba ya sala hiyo waislamu
walisisitizwa kuimarisha umoja na kuendeleza amani iliyopo sambamba na
kufuata mafunzo ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Baada
ya hapo Rais Dk. Shein alifika Ikulu mjini Zanzibar na kupata fursa ya
kusalimiana na viongozi wa Dini ya Kiislamu na baadae aliwapa wananchi
waliofika katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar skukuu yao ya Idd El
Fitri kama ilivyo kawaida yake kwa miaka yote kila ifikapo siku hii.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Alhajj Ali
Mohamed Shein, akishiriki katika Ibada ya Sala ya Eid Fitry iliofanyika
katika viwanja vya Maisara Suleiman leo, baada ya kumalizika kwa mfungo
wa Mwezi Mtuku wa Ramadhani,(Picha na Ikulu)
WAUMINI
wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatiula hutba ya Sala ya Eid Fitry
katika viwanja vya Maisara Suleiman leo ikisomwa na Sheikh Khamis Gharib
Khamis.(Picha na Ikulu)
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akisikiliza Hutba ya Sala ya Eid Fitry baada ya kumalizika kwa
Sala hiyo iliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman, kushoto
Sheikh Abdalla Talib, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif
Ali Iddi na kulia Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi.(Picha
na Ikulu)
WAUMINI
wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatiula hutba ya Sala ya Eid Fitry
katika viwanja vya Maisara Suleiman leo ikisomwa na Sheikh Khamis Gharib
Khamis.(Picha na Ikulu)
WAUMINI
wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatiula hutba ya Sala ya Eid Fitry
katika viwanja vya Maisara Suleiman leo ikisomwa na Sheikh Khamis Gharib
Khamis.(Picha na Ikulu)
WAUMINI
wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatiula hutba ya Sala ya Eid Fitry
katika viwanja vya Maisara Suleiman leo ikisomwa na Sheikh Khamis Gharib
Khamis.(Picha na Ikulu)
MZEE
Khatib akifutilia hutuba ya Sala ya Eid Fitry katika viwanja vya
Maisara Suleiman leo baada ya kumalizika kwa sala hiyo.(Picha na Ikulu)
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akiitikia dua ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Hassan Othman Ngwali katika viwanja vya Maisara Suleiman baada ya
kumalizika kwa Sala ya Eid Fitry leo. kushoto Sheikh Abdalla Talib na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi na kulia
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi.(Picha na Ikulu)
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akiitikia dua ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Hassan Othman Ngwali katika viwanja vya Maisara Suleiman baada ya
kumalizika kwa Sala ya Eid Fitry leo. kushoto Sheikh Abdalla Talib na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi na kulia
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi.(Picha na Ikulu)
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akiitikia dua ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Hassan Othman Ngwali katika viwanja vya Maisara Suleiman baada ya
kumalizika kwa Sala ya Eid Fitry leo. kushoto Sheikh Abdalla Talib na
kulia Sheikh Saleh Omar Kabi.(Picha na Ikulu)
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akisalimiana na Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dkt. Amani Karume
baada ya kumalizika Sala ya Eid Fitry katika viwanja vya Maisara.(Picha
na Ikulu)
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein akimsalimia Mtoto Abdalla Waziri baada ya kumalizika kwa Sala ya
Eid Fitry katika viwanja vya Maisara Suleiman leo asubuhi.(Picha na
Ikulu)
No comments :
Post a Comment