Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia
akikagua kivuko cha MV. Pangani II kilichokuwa kinafanyiwa ukarabati mkubwa.
Kivuko hicho kilihamishwa kutoka Utete Wilaya ya Rufiji ambapo kilikua kinatoa
huduma kati ya Utete na Mkongo katika mto Rufiji. Kushoto ni Meneja wa TEMESA
mkoa wa Tanga Mhandisi Margareth Gina.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati
akikagua injini ya kivuko cha MV. Pangani II ambacho kilihamishwa kutoka Utete Wilaya
ya Rufiji. Kivuko hicho kimefanyiwa ukarabati mkubwa na kinatarajiwa kuanza
kutoa huduma hivi karibuni katika mto Pangani kati ya Pangani na bweni, kushoto
ni Meneja wa TEMESA mkoa wa Tanga Mhandisi Margareth Gina na kulia ni Mkuu wa
Kivuko cha Pangani Mhandisi Abdulrahman Ameir.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto akikagua chumba cha kuhifadhia vipuri vya magari na vifaa vya matengenezo kinga katika karakana ya TEMESA mkoani Tanga. Katikati ni Meneja wa TEMESA mkoa wa Tanga Mhandisi Margareth Gina na kulia ni mhasibu Martin Joram.
No comments :
Post a Comment