Monday, June 10, 2019

TANAPA WAIKABIDHI TUZO ILIYOSHINDA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI KWA WAZIRI KIGWANGALLA .

Kamishina wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akipiga saluti wakati akimpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangalla alipowasili katika viwanja vya TGT yalipofanyika maonesho ya Utalii ya Karibu/Kili fair kwa ajili ya kupokea tuzo iliyototolewa kwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti .kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara ,Adam Malima na  kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TANAPA,Jenerali Mstaafu ,George Waitara.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangalla akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea Tuzo iliyotolewa kwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,Hafla iliyofanyika viwanja vya TGT yalipofanyika maonesho ya Utalii ya Karibu/Kili fair.
Baadhi ya Makamishna wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakifuatilia tukio hilo katika viwanja vya TGT jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Prof Adolf Mkenda akizungumza wakati wa hafla hiyo sababu za Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupata tuzo hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu ,George Waitara akizungumza katika Hafala hiyo.
Mkurugenzi wa Vyombo vya Habari vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi ,Faustine Sungura ni miongoni mwa wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Wawakilishi wa Benki ya NMB pia wameshiriki  katika hafla hiyo.
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi tuzo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ,Jenerali Mstaafu ,George Waitara ili aikabidhi kwa Waziri ,Dkt Kigwangalla 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ,Jenerali Mstaafu ,George Waitara  akikabidhi tuzo iliyotolewa kwa Hidahi ya Taifa ya Serengeti kwa Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Kigwangalla wakati wa hafla fupi iliyofanyika  katika viwanja vya TGT jijini Arusha.  
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mara ,Adam Malima .mkoa ambao kwa kiasi kikubwa eneo la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti linapatikana akatoa ombi la tuzo hiyo kufikishwa pia katika mkoa wa Mara ili wananchi wapate fursa ya kuishuhudia kwa karibu.
Wanamuziki wa Bendi ya Spanest wakitumbuiza katika hafla hiyo.
Baadhi ya Makamishana wa Hifadhi za Taifa na  Mamlaka ya Ngorongoro wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Malisili na Utalii,Dkt Hamis Kigwangalla.
Na Dixon Busagaga wa Globuya Jamii,Kanda ya Kaskazini 
 
MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali  Mstaafu wa Jeshi ,George Waitara leo amekabidhi kwa Waziri wa Utalii na Maliasili  Dkt Khamis Kigwangalah tuzo iliyoshinda Hifadhi ya Taifa ya Serengeti baada ya kutangazwa hifadhi bora barani Afrika. 
Tuzo hiyo iliyotolewa na taasisi ya World Travel Award (WTA) June Moshi nchini Mauritius baada ya Hifadhi ya Serengeti kuwa na sifa za kipekee miongoni mwao ikiwa ni idadi kubwa ya wanyama wahamao,wanayama walao nyama  na uwepo wa ukanda mrefu wwenye wanyama wengi imepangwa kukabidhiwa kwa raisi Dkt John Magufuli .
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi tuzo hiyo kwa Waziri Kigwangala,hafla iliyofanyika katika viwanja vya TGT yanapofanyika maonesho ya Utalii ya Karibu/Kili fair  ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugnzi TANAPA ,George Waitara amesema ushindi wa Hifadhi ya Serengeti kuwa Hifadhi Bora ni ushindi wa Watanzania wote.
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof Adolf Mkenda amesema tuzo hiyo imepatikana baada ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushindanishwa na Hifadhi nyingine kubwa tano barani Afrika kwa watalii kupiga kura.
Mwisho 

No comments :

Post a Comment