Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji kutoka
Wizara ya Maji George Mvomera katikati akitazama kikundi cha utunzaji wa
mazingira cha Uwamakizi wakati ametembelea vikundi vya Uwamakizi na
kuona namna wanavyotunza vyanzo vya maji katika eneo dogo la Bonde la
Mto Zigi wilayani Muheza huku akiridhishwa na juhudu zilizofanywa na
Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga UWASA)
pamoja na mradi wa kunusuru vyanzo vya maji (SLM) kushoto ni Mkurugenzi
wa Mazingira Wizara Maji Obadia Kibona.
Mratibu wa mradi wa kunusuru vyanzo vya
maji kupitia matumizi bora ya ardhi (SLM) Mhandisi Maximilian Sereka
ambapo alisema mradi huo ulianza mwaka 2016 sasa wapo ndani ya mwaka wa
nne kwenye utekelezaji wa mradi huo.
Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji kutoka
Wizara ya Maji George Mvomera kulia akiangalia miti aina ya mitiki
iliyopandwa kwenye Kijiji cha Sembekeza wilayani Muheza wakati
alipotembela vikundi vya uwamakizi na kuona namna wanavyotunza vyanzo
vya maji katika eneo dogo la Bonde la Mto Zigi wilayani Muheza huku
akiridhishwa na juhudu zilizofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri
wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) pamoja na mradi wa kunusuru
vyanzo vya maji (SLM).
Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji kutoka
Wizara ya Maji George Mvomera katikati akionyeshwa namna miti ya mitiki
inavyopandwa wakati alipotembela vikundi vya uwamakizi na kuona namna
wanavyotunza vyanzo vya maji katika eneo dogo la Bonde la Mto Zigi
wilayani Muheza huku akiridhishwa na juhudu zilizofanywa na Mamlaka ya
Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) pamoja na
mradi wa kunusuru vyanzo vya maji (SLM).
Mtaalamu wa Mazingiwa Tanga Uwasa
Ramadhani Nyambuka kushoto akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa
Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera
Mhandisi Rashid kutoka Tanga Uwasa kushoto akiwaongoza wataalamu mbalimbali
Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera akitazama namna miche ya matikiti inavyopandwa
Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufika kwenye ofisi za Umoja wa Wakulima Wahifadhi wa Mazingira Kihuhwi Zigi
Kikundi cha Uwamakizi kikitoa burudani
Sehemu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali
Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji kutoka
Wizara ya Maji George Mvomera kwenye shuti nyeusi katikati akiwa kwenye
picha ya pamoja na kikundi cha Uwamakizi
**
Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji kutoka
Wizara ya Maji George Mvomera ametembelea vikundi vya uwamakizi na kuona
namna wanavyotunza vyanzo vya maji katika eneo dogo la Bonde la Mto
Zigi wilayani Muheza huku akiridhishwa na juhudu zilizofanywa na Mamlaka
ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) pamoja
na mradi wa kunusuru vyanzo vya maji (SLM).
Mradi huo unasimamiwa na Wizara ya Maji
chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
ambao umeweza kusaidia utunzaji wa vyanzo vya maji ikiwemo upandaji wa
miti kwenye maeneo husika na hivyo kufanya maeneo hayo maji kutiririka
mwaka mzima.
Akizungumza mara baada ya kutembelea
eneo hilo ikiwa ni wiki ya mazingira, Mvomera alioneshwa kuridhishwa na
utunzaji wa mazingira unaofanywa na Uwamakizi huku akiwataka wananchi
kote nchi kujiunga kwenye vikundi vinavyojihusisha na namna ya kutunza
mazingira kwenye vyanzo vya maji ikiwemo kupanda miti rafiki inayotunza
maji katika kipindi cha kiangazi.
Alisema wameona kazi kubwa na nzuri
inayofanyika kwenye eneo hilo kwani miaka ya nyuma mito hiyo ilikuwa
haititirishi maji lakini sasa hivi kutokana na uwepo wa utunzaji wa
mazingira maji yameanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida na hilo ndio
lengo lao nchi nzima wananchi wajiunge kwenye vikundi na kujihusisha na
namna ya kutunza mazingira leo.
“Lakini katika kusheherekea wiki ya
mazingira lengo la mwaka huu ni kuhamasisha wananchi kmuacha kutumia
mifuko ya plastic lakini pia tumejifunza mengi zaidi miti inayopandwa
lazima iweze rafiki kwenye utunzani wa vyanzo vya maji kwani inachangia
uwepo wa maji kwenye mito kipindi cha kiangazi”Alisema.
Mkurugenzi huyo alisema miti hiyo
inasaidia kufanya mito kutiririsha maji mwaka mzima kwenye maeneo ya
vyanzo hizyo huku akikipongeza kikundi cha Uwamakizi kwa kuhifadhi
mazingira na Mto Zigi na mito mingine midogo inayoingiza maji kwenye mto
huo.
Aidha alisema pia wanategemea kuanzisha
mfuko wa maji (Water Fund) kwenye eneo la Uwamakizi kwa kushirikiana na
Tanga Uwasa na wadau wengine kuunda mfuko huo ili mradi huo uwe endelevu
uhifadhi wa mazingira uendelea kwenye maeneo mengi zaidi ya bonde dogo
la mto Zigi ambayo ni sehemu ya bonde la Mto Pangani.
“Niwapongeza uwamakizi kwa kazi nzuri
wanayoifanya lakini nitoe wito maeneo mengine Tanzania waende kujifunza
uwamakizi namna ya kutunza vyan zo vya maji namna inavyoileta faida kwa
wananchi wanalima kokoa mitiki inayowezesha kujiongeza kipato na kutunza
maji kwa kupanda mazao mbadala ya mahindi na maharage ambayo yangewezea
kuharibu vyanzo hivyo”Alisema.
Hata hivyo alisema Wizara ya Maji
imekuwa ikisaidia maeneo mengi kuanzisha vyama vya watumiaji wa maji kwa
nguvu ya wizara maeneo mengine wa usafiri na ofisi faida za jumuiya za
watumiaji maji zinasaidia kutatua changamoto za utunzaji wa maji na
mazingiea eneo la uwamakizi watafanya kila njia kuwatafutua usafiri wa
pikipiki kwa sababu ni eneo kubwa kupitia mradi wa kunusuru.
Naye kwa upande wake Mratibu wa mradi wa
kunusuru vyanzo vya maji kupitia matumizi bora ya ardhi (SLM) Mhandisi
Maximilian Sereka alisema mradi huo ulianza mwaka 2016 sasa wapo ndani
ya mwaka wanne kwenye utekelezaji wa mradi huo.
Alisema mradi huo unatekelezwa na
serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Maendeleo Dunia
(UNDP) pamoja na Mfuko wa Mazingira (GF) kwa kipindi cha miaka minne ya
utekelezaji kwa kushirikiana na sekta mbalimbali wamepata mafanikio
mengi ikiwemo utoaji wa elimu kwenye maeneo yote mawili Ruvu na Zigi
hivyo kuwafanya wananchi kuwa na uelewa mkubwa ukilinganisha na kipindi
wanaanza mradi.
Mratibu huyo alisema pia kumekuwepo na
ushirikianao kwenye sekta mbalimbali wakati wa utekelezaji wa mradi huo
ambao unaratibiwa na sekta ya maji kwa kushirikiana ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira, Wizara ya Kilimo,Mifugo,
“Lakini pia sekta za serikali mbalimbali
ikiwemo mamlaka za maji ya Tanga Uwasa,Moruwasa na Dawasa lakini pia
wilaya mbalimbali wanazoshirikiana nazo kwa ukaribu zaidi wilaya za
Tanga na Morogoro”Alisema
No comments :
Post a Comment