Friday, June 28, 2019

KAMPUNI YA WE FARM YAZINDUA HUDUMA YA WAKULIMA KUBADILISHANA TAARIFA KUPITIA UJUMBE WA SIMU ZA MIKONONI

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo na Chakula, Bwana Beatus Malema, akiwa na Meneja Mkuu wa We Farm, Bw. Nicholaus John (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Kusaidia Wakulima cha taasisi ya We Farm, Bi.CyrilaAnthony, akizinduan huduma hiyo kwa kugusa nembo (logo) ya taasisi hiyo kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Juni 28, 2019.
Mkuu wa Kitengo cha Kusaidia Wakulima cha taasisi ya We Farm, Bi.CyrilaAnthony, akitoa hotuba yake.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo na Chakula, Bwana Beatus Malema
Meneja Mkuu wa We Farm, Bw. Nicholaus John akitoa hotuba yake. Meneja Mkuu wa We Farm, Bw. Nicholaus John akitoa hotuba yake.
Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
TAASISI ya tunalima WE FARM imezindua mfumo wa kuwawezesha wakulima  kubadilishana taarifa kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia simu za kiganjani.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua mfumo huo kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo Juni 28, 2019, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo na Chakula, Bwana Beatus Malema amesema, mfumo huo utawezesha kusaidia njia inayotumiwa kwa sasa ya kuwaelimisha wakulima kwa kutumia Maafisa ugani.
“Mfumo huu lengo lake ni kutengeneza mtandao wa mawasiliano na utawezesha wakulima kuweza kutuma ujumbe wowote ili kuuliza chochote kuhusu shamba lake au katika eneo lake la kazi na majibu yatatolewa papo hapo.” Alifafanua Bw. Malema.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa WE FARM , Bw.Nicholaus John alisema huduma hiyo ni bure na mkulima atatuma ujumbe mfupi kupitia namba 15088.
“Mkulima ataweza kuuliza maswali na kupata majibu kutokana na matatizo mbalimbali yaliyopo shambani wkake, wazo hili lilikuja kutokana na kwamba wakulima wanachangamoto nyinginmashambani lakini wanakosa habari au ujuzi wa kuweza utatua matatizo yao.” Alisema na kuongeza….Kinachofanywa na WE FARM ni kumuwezesha mkulima kuuliza swali na kupata majibu kutoka kwa wakulima wenzake na hivyo kumuwezesha kuendelea na kilimo chake kwa njia iliyo sahihi.” Alisema

No comments :

Post a Comment