Amewataka
pia wamiliki hao waache mara moja kuwalea watoto hao katika maadili
yasiyofaa na yasiyo ya Kitanzania na kwamba maofisa ustawi wa jamii
wahusike moja kwa moja katika usajili wa mtoto ili kuhakikisha kuwa ni
watoto wanaostahili tu kuwekwa kwenye makao ndiyo wanasajiliwa.
Alikuwa
akizungumza jana usiku (Jumapili, Mei 26, 2019) kwenye Viwanja vya
Karimjee, jijini Dar es Salaam alikokuwa mgeni wa heshima wakati wa
futari ya pamoja na watoto yatima kutoka kwenye vituo sita vya kulea
watoto yatima vya jijini humo.
“Nitoe
rai kwamba watu mmoja mmoja, taasisi na makao wazingatie baadhi ya
taratibu za msingi za uendeshaji wa makao kama vile mtoto kukuzwa katika
mazingira ya familia, kuzingatia misingi ya kitaifa badala ya misingi
ya tamaduni za kigeni.
“Mtoto
kukuzwa kwa kuzingatia maslahi bora ya mtoto; kuzingatia umuhimu wa
kuwa na mwendelezo katika dini ya mtoto na utamuduni wake;
kutotenganisha watoto na ndugu na kuhakikisha watoto wote wanapata
huduma stahiki, kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji; na
kutunzwa na kuendelezwa hadi kufikia kimo cha utimilifu wao,” alisema.
Waziri
Mkuu alitumia hadhara hiyo pia kutoa maelekezo mahsusi kwa waendeshaji
wa makao pamoja na wasimamizi wa sheria na taratibu za uendeshaji wa
makao ya watoto yatima.
“Afisa
Ustawi wa Jamii katika eneo yanakoanzishwa makao, ahusike moja kwa moja
katika usajili wa mtoto ili kuhakikisha kuwa ni watoto wanaostahili tu
kuwekwa kwenye makao ndio wanasajiliwa.
“Taasisi
na makao zihakikishe kuwa kila mtoto anawekewa mpango maalumu wa
kuondoka kwenye makao na namna ya kumuunganisha mtoto huyo na familia
yake.
“Wamiliki
wa taasisi na makao, waruhusuni maafisa ustawi wa jamii na maafisa
wengine wa Serikali wafanye ukaguzi kwa mujibu wa sheria na wekeni
utaratibu wa kuandaa taarifa za kila mwezi za watoto na taarifa ya mwaka
wa fedha,” alisema Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu pia alionya dhidi ya wale “wanaowabadili watoto dini kinyume cha
sheria; wanaofanya vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto;
wasiowaruhusu watendaji wa Serikali kufanya ufuatiliaji na usimamizi;
wasioandaa mpango wa kuwaunganisha watoto na familia zao na hivyo,
kusababisha watoto kukaa kwa muda mrefu kwenye makao na wale wote
wanaondesha makao bila kuwa na leseni ya uendeshaji.”
Alisema
Serikali haitowafumbia macho watu wa namna hiyo, na mara tu
watakapogundulika kuanzisha au kuendesha makao bila kufuata taratibu,
hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Alisema
tangu mwaka 2016 hadi sasa, kuna jumla ya watoto 24,067 wanaolelewa
katika makao yaliyosajiliwa nchini yakiwemo makao 140 yanayoendeshwa na
kumilikiwa na watu au taasisi binafsi. Kati yao wavulana ni 11,925 na
wasichana ni 12,142.
Alisema
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto inaratibu upatikanaji wa huduma za msingi kwenye makao kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali. Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na
kuwezesha upatikanaji wa Bima ya Afya kwa watoto wanaoishi katika
mazingira hatarishi. “Hadi sasa, watoto 900 kutoka Dar es Salaam, Mbeya,
Kilimanjaro na Arusha wamepatiwa kadi hizo na zoezi hilo linaendelea,”
alisema.
Waziri
Mkuu alisema Serikali itaendelea kusimamia na kufuatilia kwa karibu
uendeshaji wa makao ya watoto sambamba na kutoa elimu kuhusu malezi,
makuzi, haki, ulinzi na usalama wa mtoto kwa mujibu wa sheria
zinazosimamia haki na ustawi wa mtoto.
Mapema,
akielezea azma ya kuandaa futari hiyo, Mkurugenzi wa Chocolate Princess
na mwandaaji wa kipindi cha televisheni maarufu cha The Mboni Talk
Show, Bi. Mboni Masimba alisema jumla ya watoto yatima 325 walikuwa
wamealikwa kushiriki futari hiyo.
Watoto
hao wanatoka vituo vya Ijango Zaida Orphanage Centre kilichopo Sinza,
Alzama Orphanage Centre (Mbagala), Ashura Foundation (Vingunguti),
Madina Orphanage Centre (Tandale), Hiyari Orphanage Centre (Mbagala) na
Hisani Orphanage Centre (Mwasonga).
Futari
hiyo iliandaliwa na Mboni Masimba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
wakiwemo Asure Yetim Vafki, United Bank of Africa (UBA), Junaco, Mo
Dewji Foundation, Lake Oil, ASAS, AZAM, Uncle K Catering, Zurii, Simply
Special Decor na State Oil na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo
Balozi wa Uturuki nchini, Bw. Ali Davutoğlu, Mjumbe wa Baraza la Ulamaa
Taifa, Sheikh Issa Othman, masheikh, maimamu wa misikiti na viongozi wa
taasisi zinazojihusisha na malezi ya watoto yatima.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
No comments :
Post a Comment