Wednesday, May 29, 2019

WAZAZI WASAIDIENI MABINTI ZENU WANAPOKUWA KENYE HEDHI





NA VERO IGNATUS, ARUSHA
MZUNGUKO wa siku ya hedhi kwa wanawake limekuwa ni jambo halizungumzwi hadharani  katika jamii nyingi barani Afrika

kutokana na tamaduni na imani za kidini.

Mwaka 2015 Kwa mara ya kwanza Tanzania iliungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya hedhi ambapo jamii inaelimishwa kuhusiana na jambo hilo ambalo ni la kawaida katika mfumo wa maisha ya mwanamke kila baada ya wastani wa siku 28.

Pia mwaka huu 2019 Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku hiyo ambapo mwaka huu kauli mbiu ya siku hiyo inasema “Ni wakati wa kuchukua hatua”.

Wakati dunia inapoadhimisha siku ya usafi wa hedhi, bado wasichana na wanawake wengi wanakabiliwa na changamoto ya kupata taulo za kike (Pedi ) wakati wa hedhi hivyo kufanya usafi wakati huo kuwa vigumu

Katika maadhimisho yaliyofanyika jijini Arusha wananchi na wataalamu mbalimbali wa afya wameizungumzia siku hiyo ikiwa ni pamoja na kueleza wajibu wa jamii kukabiliana na changamoto zinazowakuta wanawake na hususan wasichana wa shule kuweza kumudu gharama za kununua taulo hizo za kike.
Dkt.Janeth Fussi kutoka hospital ya Shash iliyopo Zanzibar Mkoa wa mjini Magharibi amesema vipo vitu vinavyotakiwa kufanya kipindi hicho ni

usafi wa mwili kwa ujumla, kufanya mazoezi madogomadogo, pamoja na kula mbogamboga na matunda kwa wingi kipindi chote cha hedhi

Aidha Dkt. Fussi amesema yapo makatazo vitu visivyotakiwa kufanywa katika kipindi cha hedhi ikiwa ni pamoja na kukaa na taulo za kike kwa muda mrefu kwani huleta hatari ya kupata maambukizi kama fangasi lakini pia inashauriwa kutokufanya tendo la ndoa katika kipindi hicho.

Alisema zipo Changamoto nyingi katika kipindi cha hedhi ambapo wengine wanapata maumivu makali ya tumbo,


baadhi hupata kichefuchefu maumivu ya kiuno au mgongo na wengine huwa na hasira.Jane Edward ni Mwenyekiti wa Taasisi ya VIPATU Mkoa wa Arusha anasema jamii nyingi hususani wasichana na wanafunzi wengi huwa wanakabiliwa na ukosefu wa nguo za ndani za kutosha “Unakuta mtoto wa kike amenunuliwa chupi mbili anavaa kwa muda mwingi lakini katika kipindi cha hivi karibuni, tunashuhudia wadau wa wanafunzi hao kupeleka taulo za kike mashuleni, bila kuzingatia kuwa, taulo hizo ni budi ziendane na zinaendana na nguo za ndani (chupi).
Hata hivyo ameshauri wadau waendelee kujitolea taulo hizo za kike lakini wasisahau kuwa “Taulo hizo  hizo lazima ziwekwe kwenye chupi, ambazo watoto wengi hawana chupi  bora ila wana bora chupi.” Alisema Bi. Jane Edward
Waridi Ally (siyo jina lake halisi) Ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule moja wapo jijini hapa anasema anapopata hedhi, hawezi kuketi darasani, kwa sababu hakuna pedi au sod yeye huenda nyumbani na kutengeneza vitambaa na kuvaa.
"Wasichana wengi tunakosa ujasiri wa kusimama na kujibu maswali darasani haswa tukiwa mchanganyiko na wavulana tunahisi kuchafuka hivyo tunaona aibu mara zote,wazazi wetu wengine hawana uwezo wa kutununulia"
Julius Mungaya ni Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Arusha na pia ni mzazi amesema ni vyema jamii ikatoa elimu kwa watoto wao wa kike kujitambua na kujielewa na kuwa na vifaa vitakavyowasitiri kwenye siku yao hiyo muhimu

Amesema pamoja na kujielewa mabinti wanapaswa kutambua umuhimu wa usafi kwa kuepuka magonjwa na maradhi yatokanayo ma uchafu.
"Inafahamika kuwa wanawake hawapendi uchafu haswa kipindi cha hedhi" alisema
Ameomba mashirika ya serikali na yasio ya kiserikali kupita mashuleni na kutoa elimu kwa mabinti ya kujitambua na kufahamu nn maana ya usafi Katika kuadhimisha siku ya Hedhi duniani
Eliphace Laizer ni Msimamizi wa Kituo cha Radio Habari Maalum anasema kuwa Jambo hilo la hedhi lisifanywe kuwa ni Jambo siri kwa wanawake hasa wenye umri mdogo.
Wengi wamekuwa wakificha wakifikiri ni Siri na kujikuta wanaacha kuhudhuria shule kwa kisingizio cha kuwa wagonjwa.
Pia niombe serikali iangalie namna ya kuboresha miundo mbinu kwa kuwatengea vyumba maalum kwa watoto hawa wawapo katika kipindi hiki.

No comments :

Post a Comment