Friday, May 3, 2019

VIONGOZI WA DINI, SIASA NA KIMILA WASHIRIKISHWE KUELIMISHA JAMII KUZUIA VIFO VITOKANAVO NA UZAZI-RC MTAKA


PICHA 1
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, uliofanyika  Tuwavushe Salama, Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
picha 2
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wadau wa afya  baada ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
picha 4
Baadhi ya viongozi na wadau wa afya Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
picha 5
Kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Makamu Mwakiilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) hapa nchini, DKT. Hashina Begum  na Mratibu wa UNFPA Mkoa wa Simiyu, Dt. Amir Batenga wakiteta jambo wakati wa hafla ya  Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
picha 6
Makamu Mwakiilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) hapa nchini, DKT. Hashina Begum akizungumza na viongozi na wadau wa afya Mkoani Simiyu,wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
picha 7
Baadhi ya viongozi na wadau wa afya Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
picha 8
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dinna Atinda akizungumza na viongozi na wadau wa afya Mkoani Simiyu,wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
picha 9
Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Mageda Kihulya akiwasilisha taarifa ya hali ya vifo vya wanawake na  watoto, wakati wa hafla ya  Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama, uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
……………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa
Serikali mkoani hapa kuona umuhimu wa kuwashirikisha viongozi wa dini, siasa na wa kimila katika utoaji wa elimu kwa jamii na kuwahamasisha wanawake wajawazito kuhudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi..
Mtaka ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uwajibikaji  katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kama JIONGEZE, Tuwavushe Salama uliofanyika  Mei 02, 2019 Mjini Bariadi.
“ Ni vizuri tukaongeza wigo wa kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa mama wajawazito  kuhudhuria kliniki kipindi cha ujauzito na kuhakiksha wanajifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya; viongozi wa dini,siasa na wa kimila wana nafasi kubwa kwenye jambo hili muone namna ya kuwashirikisha “ alisema  Mtaka.
Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya ikiwa ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) imeboresha vituo vya kutolea huduma, hivyo ni vema jamii ikaelimishwa umuhimu wa kutumia huduma za afya ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Katika hatua nyingine Mtaka ameishukuru UNFPA kwa namna ilivyosaidia katika ujenzi wa miundombinu ya afya,vifaa na vitendea kazi kama magari ya kubeba wagonjwa huku akisisitiza viongozi na watendaji walioshiriki katika uzinduzi wa kampeni hii kutoka na dhamira ya kuwavusha salama akina mama wajawazito na watoto na kupinga vifo vitokanavyo na uzazi..
Mwakilishi wa  Ofisi  ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dinna  Atinda ameusisitiza uongozi wa mkoa  kusimamia vituo vinavyotoa huduma za afya za msingi na dharura kuhakikisha vinatoa huduma bora kwa wananchi.
Naye Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Salome Mwijuma  ametoa wito  kwa jamii kuendelea kuwasaidia wanawake wajawazito waweze kuhudhuria kliniki muda wote, wapate lishe bora na kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma ili wajifungue salama.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Mageda  Kihulya amesema mwaka 2015 watoto 680 walifariki na mwaka 2018 watoto 640 walifariki,  wakati kwa upande wa akina mama wanaojifungua vifo vimepungua kutoka 48 mwaka 2015 na kufikia 40 mwaka 2018,  jambo ambalo linaonesha kuwa nguvu ya ziada kutoka wadau mbalimbali inahitajika kumaliza tatizo hili.
Dkt. Mageda amesema sababu zinazosababisha vifo vingi vya akina mama wajawazito kama vile kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua na mkingamo wa uzazi zinaweza kuzuilika, hivyo akatoa wito kwa wakina mama kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma kuzuia vifo hivyo, huku akisisitiza watoto chini ya miaka mitano nao wapewe chanjo kuzuia vifo..
Makamu Mwakilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) hapa nchini, Dkt. Hashina Begum amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika jitihada mbalimbali za kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto

No comments :

Post a Comment