Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb.) akihutubia kwenye kuadhimisha siku ya
Taifa la Uholanzi, kulia ni Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jeroen
Verheul.
Prof. Palamagamba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo
alitumia fursa hiyo kuelezea mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania
na Uholanzi katika sekta mbalimbali zikiwemo Kilimo, Elimu, Biashara na
Ujenzi wa Miundombinu. Pia alilipongeza taifa hilo kwa kuendelea
kushirikiana na Tanzania kwenye kuleta maendeleo nchini.
Aidha, Prof. Kabudi alieleza kuwa Tanzania inaendelea kuboresha
mazingira ya uwekezaji ili kuwavutia wawekezaji wa Uholanzi kuja
kuwekeza nchini kwa wingi, ambapo alieleza kuwa mpaka sasa Uholanzi ni
miongoni mwa nchi 10 zinazoongza kwa uwekezaji nchni, ambapo imewekeza
jumla ya miradi 159 Tanzania.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt.
Mohamed Gharib Bilal, Mabalozi mbalimbali wanao ziwakilisha nchi zao
hapa pamoja na wawakilishi wa mashirika ya Kimataifa. |
No comments :
Post a Comment