Naibu Spika wa Bunge Mh. Tulia
Ackson akimaliza mbio za kilomita 5 huku akiwa ameongozana Mabalozi wa
Tulia Ackson Marathon Babu Tale kushoto Meneja wa mwanamuziki Diamond
Platnumz na Msanii Izo Busness huku akishangiliwa.
Mbio za (Tulia Marathon 2019)
zinafanyika jijini Mbeya zikianzia kwenye uwanja wa Sokoine na
kumalizikia uwanjani hapo ambapo kumefanyika mbio za kilomita 42,
Kilomita 21, Kilomita 5 na Kilomita 2 , Mbio hizo zimeshirikisha
wanariadha kutoka Kenya na hapa nchini.
Naibu Spika wa Bunge Mh. Tulia
Ackson akishiriki mbio za kilomita 5 na Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini
Mh. William Ntinika pamoja na baadhi ya wabunge.
Naibu Spika wa Bunge Mh. Tulia Ackson akivishwa nishani mara baada ya kumaliza mbio za kilomita .
Baadhi ya wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania pia wameshiriki katika mbio hizo za (Tulia Marathon 2019).
Baadhi ya viongozi mbalimbali walioshiriki katika mbio hizo wakijiandaa kuanza mbio hizo kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mbunge wa jimbo la Mbarali Mh.
Haroun Pre Mohamed akimaliza mbio za Tulia Ackson 2019 kilomita 5
kwenye uwanja wa Sokoine zilizofanyika leo jijini Mbeya
Mbunge wa jimbo la Mbarali Mh.
Haroun Pre Mohamed akivishwa nishani mara baada ya kumaliza mbio za
Tulia Ackson 2019 kilomita 5 kwenye uwanja wa Sokoine zilizofanyika leo
jijini Mbeya
Baadhi ya washiriki wakimalizia mbio za (Tulia Marathon 2019) Kilomita 5
Mbunge wa jimbo la Mbinga Mh.
Sixtus Mapunda na Cosato Chami wa jimbo la Mafinga wakimalizia mbio za
(Tulia Marathon 2019) Kilomita 5.
Na hawa nao walishiriki mbio za kilomita 5
Mbunge wa jimbo la Mbinga Mh. Sixtus Mapunda na Cosato Chami wa jimbo la Mafinga wakijiandaa na mbio hizo.
Rais wa Chama cha Riadha na Mkuu
wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka na Naibu Spika wa Bunge Mh. Tulia
Ackson wakijiandaa kwa mbio hizo kulia ni Mbunge wa vitimaalu CCM mh.
Vick Kamata.
Naibu Spika wa Bunge Mh. Tulia
Ackson na Rais wa Chama cha Riadha RT Mh. Anthony Mtaka wakiwa katika
picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge.
Viongozi mbalimbali na wabunge wakijiandaa kwa mbio hizo.
No comments :
Post a Comment