MWILI
wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi utawasili
nchini
Jumatatu 6, 2019 na ndege ya Shirika la ndege la Emirate ukitokea Dubai,
Falme za Kiarabu, Mwanasheria wa familia ya Dkt. Mengi, Bw. Michael
Ngalo amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 3,
2019.
Mwili wa Dkt. Menghi ambaye alifariki
dunia akiwa huko Dubai usiku wa kuamkia Mei 2, 2019, ukishawasili jijini Dar es
Salaam, utahifadhiwa kwenye hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo na siku inayofuata yaani Jumanne Mei 7, 2019, shughuli ya
kuaga mwili huo itafanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini.
Taarifa
hiyo imeendelea kusema kuwa baada ya shughuli hiyo ya kutoa salamu za mwisho,
mwili wa Dkt. Mengi utasafirishwa Jumatano Mei 8, 2019 kuelekea mahala
alikozaliwa Machame, Mkoani Kilimanjaro ambapo shughuli za mazishi zitafanyika
Alhamisi Mei 9, 2019.
No comments :
Post a Comment