Monday, May 27, 2019

Breaking : LAZARO NYALANDU AKAMATWA KWENYE MKUTANO WA CHADEMA


Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amekamatwa na TAKUKURU akiwa anasimamia uchaguzi wa kata wa CHADEMA mkoani Singida.
Mkurugenzi wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, John Mrema, amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa Nyalandu amechukuliwa akiwa kwenye kikao cha chama cha ndani.
"Nyalandu alikuwa kwenye kikao cha ndani ili kuhamasisha uchaguzi wa ndani wa chama, na awali alichukuliwa na polisi hivyo tumewatuma mawakili wetu tayari kufuatilia juu hilo", amesema Mrema.
Taarifa za awali zilidai kuwa, Nyalandu amekamatwa na kuchukuliwa na watu waliokataa kujitambulisha akiwa kwenye kikao cha ndani cha CHADEMA kwenye kata ya Itaja, wilaya ya Singida vijijini mkoani Singida.
Wengine waliokamatwa ni Mwenyekiti wa kata hiyo na aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema wa jimbo hilo, David Jumbe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Sweetbert Njewike amesema taarifa hizo ni za uzushi; “Ndugu mwandishi umefanya vyema kuniuliza, watu wanazusha uongo mitandaoni, watafuteni TAKUKURU watawapa ukweli wa jambo hilo, polisi hawajamkamata.”

No comments :

Post a Comment