Mkuu
wa Wilaya ya Ilemela Dk Severine Lalika(kushoto) akipokea moja ya
kompyuta 10 kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha bia cha TBL Mwanza Patel
Kilovele, zilizotolewa na kiwanda hicho kwa ajili ya shule za msingi na
sekondari za kata ya Pasiansi jijini Mwanza, na printa tatu kwa ajili ya
kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha KKKT
Misungwi.kulia ni Meneja Raslimali Watu wa TBL Mwanza,Dora Nyambalya.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilemela Dk Severine Lalika (kushoto) akipokea moja ya
printa tatu kwa ajili ya kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika
mazingira magumu cha KKKT Misungwi na kompyuta 10 kwa ajili ya shule
za msingi na sekondari za kata ya Pasiansi jijini Mwanza,zilizotolewa na
kampuni ya bia ya TBL.
Walimu
wakuu na Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi wa kata ya Pasiansi,
wakijaza fomu ya kupokea Kompyuta 10 kutoka kampuni ya TBL kwa ajili ya
shule zao, kwenye hafla iliyofanyika jijini Mwanza.
Meneja
wa kiwanda cha TBL Mwanza Patel Kilovele akiongea wakati wa hafla
hiyo (kulia) ni Meneja Rasilimali watu wa kiwanda hicho Dora Nyambalya.
………………………
Kampuni
ya Tanzania Breweries Limited (TBL),baada ya kutoa msaada wa kompyuta
mpakato 20 kwa shule 3 tatu za sekondari mkoani Dar es Salaam,wiki hii
imetoa msaada wa kompyuta 10 na
printer 3 kwa ajili ya shule za msingi
na sekondari za kata ya Pasiansi jijini Mwanza, na printa tatu kwa ajili
ya kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha KKKT
Misungwi.
Akiongea
wakati wa kukabidhi msaada huo,Meneja wa kiwanda cha TBL cha
Mwanza,Patel Kilovele,alisema msaada huo ni mwendelezo wa kampuni
kusaidia huduma za kijamii katika maeneo ambayo inafanyia biashara zake
sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali kukabiliana na changamoto
mbalimbali.
“TBL
tutaendelea kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii ,
kwa kuwa hivi sasa tuko katika ulimwengu wa kidigitali tumeona ni vema
shule zetu nazo zipate kompyuta kwa ajili ya kurahisisha kazi na
kuboresha elimu,”alisema Kilovele
No comments :
Post a Comment