Waziri wa Mazingira Mh.
January Makamba akiongea na waandishi wa habari baada ya mkutano
uliofanyika ukumbi wa mkutano katika jengo la Millennium Tower jijini
Dar es Salaam ambapo uliwakutanisha na wadau mbalimbali kujadili namna
ya kudhibiti taka na kuwa biashara
…………………
NA EMMANUEL MBATILO
Viongozi wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam wamekutana na wadau mbalimbali wa kudhibiti taka ngumu
kwa lengo la kujadili namna ambayo wanaweza kukusanya taka na kuzifanya
kuwa
shughuli ya biashara na ajira.
Akizungumza na
wanahabari jijini Dar es Salaam, Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa
raisi, mazingira na muungano Mh. January Makamba amesema kuwa mfumo wa
ukusanyaji taka ni muhimu hasa serikali kuweka mazingira ya kisera,
kisheria na kiuchumi ili takataka ziwe mali.
“Tumeona watu
wanaokusanya taka mtaani na katika majumba yetu kila siku muda mwingine
tunaeaona kama vichaa kutokana na kuokota taka hizo ikiwemo makopo
lakini hiyo ni shughuli ya ajira na ya kipato na tunaamini kwamba
ilasimishwe”. Amesema Makamba.
Aidha Waziri huyo
amesema kuwa miundombinu ya miji lazima iboreshwe hasa wao kama serikali
wanajukumu la kuboresha miundombinu ikiwemo madampo, mifereji pamoja na
kuweka sehemu ya kutupa na kukusanya.
“Sera, sheria, kanuni na
taasisi kwamba suala la ukusanyaji wa taka na udhibiti wa taka lazima
lifanywe na taasisi mahususi kwa ujumla na lazima kuwepo na sheria
ikiwemo sheria ndogo na sera ambazo zitawezesha shughuli ya taka iwe
biashara na ifanyike kwa urahisi.
Waziri Makamba
amemalizia kwa kusema kuwa shughuli ya ukusanyaji wa taka lazima uwe
shirikishi kuanzia wanaokusanya,wanaozalisha taka na viongozi pamoja na
wasasi.
Kwa upande wa Naibu
Makamo Mkuu wa Chuo Utafiti, Profesa Cathbert Kimambo amesema mkutano
huo ambao umewashirikisha wadau wa nje na ndani watajadili na kusambaza
taarifa na matokeo ya kitafiti na yakitaalamu kuhusu masuala ya
ukusanyaji wa taka ngumu.
Vilevile upande wa
Mratibu wa kitengo cha tafiti za sera na utetezi Chuo Kikuu Dar es
Salaam shule kuu ya biashara Dkt. Goodluck Charles amesema katika tafiti
ambazo zimefanyika ni kuangalia njia za kuboresha masuala ya kukusanya,
kusafirisha na kuchakata taka ngumu katika jiji la Dar es Salaam na
katika majiji mengine.
“Tumefanya utafiti
unaohusisha teknolojia rahisi ambayo wakusanyaji taka na wengine walioko
kwenye mnyonyoro wa thamani wa taka wanaweza kuzitumia ili kuboresha
thamani ya taka na kuona taka ni mali “. Amesema Dkt. Charles.
No comments :
Post a Comment