Waziri wa Maji, Mhe. Profesa
Makame Mbarawa akiwa kwenye moja ya eneo la Mradi wa Maji wa Kapapa,
Halmashauri ya Busokelo mkoani Mbeya.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa
Makame Mbarawa (aliyeshika kiuno) akikagua kazi ya kuunganisha mabomba
akiwa na Mkurigenzi Mtendaji wa Kampuni ya Leostarf Engineering Ltd,
Mhandisi Johannes Mgosi waliopewa kandarasi ya ujenzi wa Mradi wa Maji
wa Kapapa uliopo katika Halmashauri ya Busokelo, mkoani Mbeya.
Sehemu ya chanzo kipya cha maji kwa ajili ya Mradi wa Maji wa Kapapa kikiwa kimekamilika.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa
Makame Mbarawa akitoka kukagua ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Chunya
Mjini uliokamilika katika Halmashauri ya Chunya, mkoani Mbeya.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa
Makame Mbarawa (katikati) pamoja na Meneja Ufundi wa Mbeya UWASA,
Mhandisi Ndele Mengo (kushoto) akiwa juu ya tenki la Mradi wa Maji wa
Chunya Mjini uliokamilika katika Halmashauri ya Chunya, mkoani Mbeya.
………………………….
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa
Makame Mbarawa amempa siku 7 mkandarasi kukamilisha
kazi ya ujenzi wa
Mradi wa Maji wa Kapapa uliopo kwenye Halmashauri ya Busokelo, mkoani
Mbeya.
Profesa Mbarawa ametoa maagizo hayo mara baada ya kutembelea mradi huo kutokana na ujenzi wake kuchelewa tangu uanze mwaka 2014.
Amesema nimekuwa sifurahishwi na mradi huu wa maji kutokutoa huduma ya maji kwa wananchi na kusababisha adha kubwa kwao.
Tatizo la mradi huu ilikuwa ni
usanifu mbovu wa chanzo hapo awali, jambo lililosababisha maji kutofika
kwenye miundombinu na kuyasambaza kwa wananchi.
Tukachukua hatua ya kumfukuza
mkandarasi na kuwakabidhi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira
Mbeya Mjini (Mbeya UWASA), ambao walimtafuta mkandarasi mwingine Kampuni
ya Leostarf Engineering Ltd na kufanya kazi ya ujenzi wa chanzo kipya
na hivi sasa amebakiza hatua ya kuunganisha mabomba 65 ya chuma kwenye
maeno yenye makorongo na kuunganisha kwenye mtandao wa wateja.
Kwa ujumla kazi inaenda vizuri na
namuagiza mkandarasi aongeze nguvu kazi, ili kila mmoja afanye kazi
katika kipande chake na baada ya siku 7 wakazi vijiji 8 waanze kupata
huduma ya maji.
Meneja Ufundi wa Mbeya UWASA,
Mhandisi Ndele Mengo amesema mradi huo utanufaisha wakazi 31,000 wa
vijiji 8 vilivyopo katika Halmashauri ya Kyela.
Katika wakati tofauti, Waziri wa
Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa amefurahishwa na kukamilika kwa Mradi
wa Maji wa Chunya Mjini na kusema mradi huo utaleta mageuzi makubwa kwa
mji huo.
Amesema mji huo umekuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji na kukamilika kwa mradi huo kumempa faraja kubwa.
Kumekuwa na hitilafu ya kiungo cha
bomba kuachia, hali iliyosababisha maji kutotoka. Lakini mpaka sasa
mafundi wanaendelea na ukarabati na baadhi ya maeneo yameshaanza kupata
maji na baada siku chache maji yatakuwa yanatoka maeneo yote
yanayohudumiwa na mradi amesisitiza Profesa Mbarawa.
Mradi wa Chunya Mjini utahudumia wakazi 15,000.
No comments :
Post a Comment