Wednesday, April 24, 2019

MILA POTOFU NDIO CHANZO CHA WATOTO WA MITAANI


Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu Manispaa ya Iringa wakiwa na mabango yanayoelezea jinsi gani wanavyo nyanyasika huko mtaani
Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu Manispaa ya Iringa
wakiwa na mabango yanayoelezea jinsi gani wanavyo nyanyasika huko mtaani
Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu Manispaa ya Iringa
wakiwa na mabango yanayoelezea jinsi gani wanavyo nyanyasika huko mtaani
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
  
MILA potofu zilizopo katika
jamii za Kitanzania zinakwamisha maendeleo ya watoto na kusababisha ongezeko la
watoto waishio na kufanya kazi mtaani.
Akizungumza na waandishi wa
habari kwa niaba ya watoto waishio kwenye mazingira magumu Bosco Nzigilwa Alisema
kuwa ubaguzi wa kijinsia kwa watoto wa kiume ambapo watoto wa kike hufanyishwa
kazi nyingi kuliko watoto wa kiume majumbani.
“Hii husababisha mtoto wa kike
kuonekana ni kama mtumishi wa shughuli za nyumbani na pia humwathiri mtoto wa
kike kisaikologia na ajione hana thamani au umuhimu katika familia kulinganisha
na mtoto wa kiume” alisema Nzigilwa 
Nzigilwa alisema kuwa mila
zinaonyesha kwamba mtoto wa kike hana sababu ya kupata elimu kwa dhana potofu
ya kuolewa,unyanyasaji wa watoto wanaoishi na kufanya kazi Mitaani.
“Watoto wanaoishi na kufanya
kazi mitaani wamekua wakinyanyaswa na jamii pamoja na vyombo vya dola vyenye
jukumu la kuwalinda,Watoto wanalawitiwa ,wanapigwa, na kubambikiziwa kesi  mbalimbali” alisema Nzigilwa 
Aidha Nzigilwa alisema kuwa unyanyasaji
wa watoto/wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari  katika vyombo vya usafiri na kumlazimisha
mwanafunzi alipe nauli sawa na mtu mzima.
“Thamani ya mtoto inapunguzwa
kwa kigezo cha kipato ikizingatiwa kuwa serikali kwa makusudi kabisa imepitisha
kiwango cha nauli kwa watoto ambacho wanaweza kukimudu lakini badala yake
baadhi ya makondakta huwalazimisha watoto
kulipa nauli ya mtu mzima, matokeo yake baadhi ya watoto huchelewa
kufika shule na wengine kushindwa kupata chakula cha mchana ili tu wamudu
kulipa nauli ya mtu mzima” alisema Nzigilwa 
Nzigilwa alisema kuwa kuwepo
kwa vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa watoto wa kike na kiume kwa visingizio
vya kupata utajiri na  kupandishwa  vyeo
au kupata nafasi mbalimbali za madaraka.
“Kwa baadhi ya familia watoto
kupigwa, kutukanwa na kuchomwa moto ,kutumikishwa  kufanya kazi ngumu, kunyimwa vyakula vyenye
virutubisho hasa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi na
kusababisha kuwa na uwezo mdogo darasani
na kuathiri makuzi yao” alisema Nzigilwa
Akijibia hoja hizo afisa ustawi
wa jamii manispaa ya Iringa Ismail Mambo alisema kuwa Serikali Imekuwa ikipata
ushirikiano kutoka kwa wadau wa watoto, Dawati la Jinsia Polisi, Mahakama,
Jamii, Walezi/Wazazi, Viongozi wa dini, Viongozi wa siasa wanatupa ushirikiano
juu ya kuwafuatilia watuhumiwa wote wanaojihusisha na vitendo vya ubakaji na
ulawiti kwa watoto
“Elimu ya Usawa wa Kijinsia
mashuleni imeendelea kutolewa kwa wanafunzi wa Shule za Msingi,Sekondari,
Awali, Chekechea kuwa waangalifu na kupokea zawadi kwa watu zaidi ya Wazazi
/Walezi wao” alisema Mambo
Mambo alisema kuwa lipo tatizo
la unyanyasaji wa watoto wanaoshi na kufanya kazi mitaani unaofanywa na jamii
inayowazuguka pamoja na vyombo vya dola. Kwa pamoja tupige kelele kwa kutoa
taarifa juu ya vitendo hivyo kwani havina nafasi katika. 
Aidha Mambo alikiri kuwepo kwa
vyombo vya usafiri ambavyo vimekuwa vikiwanyanyasa wanafunzi wakiwa  wanakwenda ama kurudi shule na kuwataka
wazazi kuwa na jukumu la kuhakikisha usalama wa watoto upo mikononi mwao.
“Mambo alisema kuwa mila na
desturi zilizopitwa na wakati  na  kama
vile  tabia ya uchoyo,mtoto
kutopata chakula cha kutosha na chenye mchanganyiko wa viini lishe hupelekea
mtoto kuwa na afya duni hivyo hivyo kuathiri uwezo wake darasani na huathiri
makuzi ya mtoto” alisema Mambo
Mambo aliwataka wazazi
tuhakikshe watoto wanapata  chakula bora
kwa ajili  ya  kukidhi
mahitaji  ya  mwili, hivyo tutapata wataalam wa fani mbali
mbali hivyo watakwenda kufanya kazi
kwenye viwanda vyetu.
“Napenda kutoa shukrani zangu
za dhati kwa  Wadau mbalimbali ambao
wamekua wakijishughulisha katika kuwahudumia watoto wetu,Taasisi mbalimbali
zinazojishughulisha  na nmasuala ya
watoto kama vile COMPASSION ,FISCH ,DAILY BREAD, HURUMA CENTRE, AMANI
CENTRE,DHI NUREYN, FARAJA HOUSE,NYUMBA YA FURAHA na  UPENDO REHABILITATION CENTRE” alisema Mambo
Mambo alimazia kwa kutoa
shukrani za pekee kwa Shirika la Iringa Development of Youth, Disabled and
Children care (IDYDC) kwa kuwezesha Maadhimisho haya kwa mwaka 2019

No comments :

Post a Comment