Monday, April 29, 2019

Kujenga uaminifu kwa umma ndiyo kazi kubwa ya wauza bima


Tokeo la picha la INSURANCE 
Na Christian Gaya

Majira Ijumaa Aprili 19, 2019
Kampuni za bima zinahitaji kuwa na uaminifu wa hali ya juu ili kupata kupata wateja wengi na hatimaye kukuza sekta ya biashara ya bima nchini. Bima ni kitu cha muhimu sana kwa ajili ya kujenga amani ya moyo, kuleta hifadhi na kulinda watu na mali zao kutokuwa na wasiwasi wowote juu ya kitu chochote kinapopatwa na janga lolote. Bima inamfanya mtu kujengeka kimapato kwa ajili ya ...
kupata mahitaji muhimu kwa siku zijazo.
Wanabima mara nyingi wao wanauza ahadi, na uaminifu ni kitu cha umuhimu sana kwa mtoa au muuzaji wa bima yeyote kuliko biashara ya aina nyingine yeyote ile. Mkataba ndio unaosema ukweli juu ya madai yanayotakiwa aliyekatiwa bima kisheria alipwe kwa kubadilishana na tozo ya bima iliyofanyika katika mkataba huo.
Mtoa bima anaahidi kulipa hasara itakayosababishwa na janga ambalo limo ndani ya mkataba. Ahadi ni kama kiashirio fulani, ambacho kilikuwa hakileti mantiki sana. Hii ina maana ya kwamba pale unaposhidwa kutimiza ahadi ya mwanzo, wasiwasi ndipo unapoanza kupanda  katika akili za watu juu ya hicho mtu kilichomjia akilini mwake. Kwa hiyo uaminifu ni jiwe la msingi mkubwa kwa biashara yeyote ile. 
Kwa bahati mbaya changamoto kubwa ambayo sekta ya bima nchini hapa inayo ni hii ya kuwa na uaminifu mdogo kutoka kwa wananchi wa Tanzania. Wakati mwingine inatokea  juu ya tofauti ya maoni mbalimbali yanayoohusiana na tafsiri za taratibu na sheria za vifungu vya bima yenyewe kati ya kampuni ya bima na mnunuzi wa huduma au bidhaa za bima na mara nyingi hutokea mpaka kushtakiana kati yao.
Mashtaki mengi yanatokea hasa wakati wa madai yanapofanyika. Mara nyingi wateja wanakuwa hawana mahali ambapo wanaweza kupeleka malalamiko na dukuduku zao. Kinachotokea ni kukata tamaa kabisa na kuamua kutokata bima ya aina yeyote tena. Na baadhi ya uzoefu mbaya unaotokea unaanza kusambaa kwenye familia na marafiki na hatimaye sekta ya bima kukosa uaminifu miongoni mwa watanzania wengi.
Ijulikane wazi ya kuwa watu wengi miongoni mwa watanzania hawajui ya kuwa kamishana wa bima ambaye ndiye msimamizi wa sekta hii ya bima na kwamba matatizo kama hayo yanaweza kupelekwa na kutatuliwa na kamishana hii yaani TIRA. Na hata wachache wanaopeleka malalamiko yao ili yatatuliwe bado wanakosa uaminifu na sekta hii na hata baada ya malalamiko yao kutatuliwa, kwa kuamini ya kuwa asingekuwa kamishna wangepoteza haki zao. Na tabia hii mara nyingi inasababisha wasikatie majanga hatarishi tena.
Hivyo, swali kubwa hapa ni, jinsi gani wauza bima wataweza kufikia kujenga na kupandisha uaminifu ndani ya soko hili ambalo liko wazi kabisa na la kutamanisha? Kwa sababu ni wauza bima wenyewe wanaoweza kurudisha uaminifu tena kwa wananchi kwa sababu wao ndio waliokuwa wameupoteza.
Kupatikana kwa uaminifu kutoka kwa umma kunahitaji kuweka wazi sifa za bidhaa, na kuwa wa ukweli na uwazi juu ya sheria, vipengele na taratibu zote na hasa kuanzia mwanzo pale kabla ya kuuziwa au wakati anapouziwa bima. Tunataka mteja aweze kungundua kipengere chochote atakachooona ya kuwa hakimfai mapema kabisa.
Kutoa habari zisizokamilika ili kumshawishi mteja anunue bima ni jambo ambalo halikubaliki hata kidogo kisheria na hapo ndipo uaminifu unapo potea kabisa na hata madai hayawezi kutambulika. Kumbuka ya kuwa thamani kubwa ya biashara ya bima ni usimamizi wa madai. Kama madai hayawezi kusimamiwa vizuri, uaminifu ndipo hapa hupotea moja kwa moja.
Jambo la pili, faida kubwa ya uaminifu inakuwa ndani ya mteja mwenyewe ambayo baadaye inaweza kujenga uhusiano wa muda mrefu n ahata kwa njia ya maneno ya mdomoni. Uaminifu katika biashara ya bima ni ya muhimu sana kwa muuza bima kuliko aina yeyote ya biashara, sababu kubwa ni kwamba kwenye bima kinachouzwa ni ahadi.
Huduma bora kwa mteja inatakiwa kutolewa hata baada ya kuuza bima/kuingia au kusaini mkataba na hasa huduma bora kwa mteja inahitaji pale madai ya bima yanapofanyika au yanapofunguliwa.
Huduma bora kwa mteja ni njia ya nyingine ya muafaka ya kujenga na kuendeleza uaminifu. Sekta ya bima inahitaji kuboresha usimamizi wa uhusiano wa mteja wa muda mrefu, kwa mfano ukichukulia faida ya kutumia njia ya digitali katika kutoa huduma bora. Uzoefu huu wa teknolojia ya habari na mawasiliano inawapa wateja na watu wengine moyo wa kujaribu kufanya mahusiano magumu ya bima kwa njia ya mtandao.
Kuwa na mazungumzo na mshauri wa masuala ya bima kwa kuongea kwa njia ya vidio juu ya jinsi ya kufungua madai inamsaidia mteja vizuri zaidi kufahamu habari waliyobadilishana, na maulizo mengi ya bima yanaweza kumalizwa kwa njia rahisi kama vile ya mazungumzo ya kwa njia ya WhatsApp.
Kama sekta ya bima inahitajika kuliangalia jambo hili kama wana bima mlichokifanya ili kumtimizia mahitaji yenu na mahitaji ya wateja wenu. Leo wateja mara nyingi wanaangalia njia bora na rahisi ya kufanya biashara. Wana bima mnahitaji kuendelea kujikumbusha nyie wenyewe juu ya mabadiliko ya mpito wa soko la bima, ya kwamba haiwekani kwa sasa kutegemea utamaduni au mfumo wa kienyeji wa jinsi ya kufanya biashara and njia za usambazaji. Mnahitaji hasa zaidi, kuwekeza kwenye ubunifu, utafiti na kujiendeleza kwenye mbinu za uuzaji ili kutoa uaminifu unaotakiwa na kuhakikisha ya kuwa biashara inakua.  

No comments :

Post a Comment