Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shrika la Kilimanjaro SAR,Ivan Brown akitoa taarifa za
shirika hilo kwa wanahabari (hawapo pichani) kuhusu shughuli
mbalimbali za uokoaji ilizofanya katika kipindi cha mwaka mmoja.
SHIRIKA la Kilimanjaro SAR linayojishughulisha na utoaji wa
huduma ya utafutaji na uokoaji wa watalii wanaopata matatizo ya kiafya katika maeneo
yenye muinuko ikiwemo Mlima Kilimanjaro limetangaza kutoa bure huduma zake kwa waongoza watalii pamoja na wapagazi .
Hatua hiyo imefikiwa baada ya baadhi ya watu wanaojishughulisha na shughuli
za kusaidia wageni katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro kupata matatizo
ya kiafya na kushindwa kupata huduma huku kundi kubwa la watu hao kukosa Bima za Afya ,wengine wakikosa kabisa kipato
cha uhakika.
Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Kilimajaro SAR,Ivan Brown
alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya shughuli
zilizofanywa na kampuni hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanza
operesheni za uokoaji kwa kutumia njia ya Helkopta.
“Sisi ni wa kwanza na pekee katika Dunia hii tunaotoa huduma
ya uokoaji Bure kwa wote wanaofanya shughuli za mlima ,tunafahamu Wapagazi,Waongoza
watalii hawana bima, hawana njia zozote za kujipatia kipato ambazo zingesaidia
katika uokoaji”alisema Brown .
“Watakaopata matatizo ya kiafya au ajali wawapo mlimani wanaweza kuwasiliana nasi ,tutaaenda
juu na kumuokoa bila ya gharama zozote kwa sababu mipango yetu ni kuokoa maisha
,ndio sababu tunasema kwa waongoza watalii au wapagazi , uhai ndio kipaumbele
cha kwanza”aliongeza Brown .
Alisema shirika hilo likiwa linaadhimisha mwaka mmoja wa
utoaji huduma katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro tayari imetoa matibabu kwa zaidi
ya watu 250 huku akieleza kuweka rekodi ya kwanza Afrika kwa kumuokoa mgonjwa
aliyekuwa katika hali mbaya ,umbali wa Mita 5000.
“ Tayari tumetoa
huduma kwa zaidi ya wagonjwa 250 na miongoni mwao aliingia kwenye historia Afrika
ya kuwa mtu wa kwanza kuokolewa kwa na Helkopta katika eneo lenye urefu wa Mita
4800 ,katika kambi ya Cosovo Mlima Kilimanjaro June 22 mwaka jana”alisema
Borown .
Kiliamanjaro SAR imeingia makubaliano na Hospitali ya St Joseph kwa kuanzisha
Kliniki ya kisasa “Kilimanjaro SAR High
Altitude Medicine Clinic” kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu kwa magonjwa
yatokanayo na muinuko .
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa shirika hilo ,Amour Abdalah
alisema kliniki hiyo ya kwanza Afrika imeanzishwa baada ya kubaini kwamba
mgonjwa anapookolewa kutoka mlimani anahitaji pia kupata huduma stahiki za matibabu
.
“Magonjwa ya mlimani yanahitaji ,matibabu maalumu ,na ndio
sababu tukaanza na operesheni ya kutoa huduma kwa kutumia Helkopta ikiwa ni
huduma ya kwanza kwa afrika na baadae mgonjwa huyu hufikishwa katika kliniki yetu
na kupatiwa matibabu”alisema Abdalah.
Alisema wazo la kuanzishwa huduma hizo lilianza mwaka 2013 baada ya kuona kwamba utoaji wa huduma sahihi
ya uokoaji na vifaa vya kitabibu vilihitajika na si pekee kwa Hifadhi ya Mlima
Kilimanjaro bali pia kwa Sekta ya Utalii Tanzania.
Abdalaha alisema kwa sasa kampuni ya Kilimanjaro SAR
imepanua wigo wa utoaji wa huduma za utafutaji na uokoaji katika maeneo mengine
zikiwemo hifadhi za taifa za Serengeti,Arusha,Manyara,Ruaha na Mikumi.
“Mlima Kilimanjaro umekuwa na wageni wengi wakifanya shughuli
za utalii ,na wengi wao baada ya kuapanda mlima Kilimanjaro wanaendelea na safari
nyingine kutizama vivutio vya utalii,jambo kubwa tunalofanya katika sekta ya
utalii ,tumewahakikishia usalama wageni wanaokuja Tanzania kupanda Mlima
Kilimanjaro “alisema Amour.
Katika kipindi cha mwaka mmoja Shirika la uokoaji ya
Kilimanjaro SAR tayari imejinyakulia tuzo tano za uongozi moja ikiwa ni ya
Tanzania ambazo ni “C.E.O of the Year 2018 Afrika “ ,“ H.R of the Year 2018 Afrika”
,“Dream Company to work for “ , “Employer Brand Afrika “ ,” Shirika Bora la kati Tanzania “ tuzo
iliyotolewa na ATE .
Mkurugenzi
wa Rasilimali watu katika shirika la Kilimanjaro SAR,Amour Abdalah
akizungumza na wanahabari (hawapo pichani kuhusu mwaka mmoja wa
operesheni ya shirika hilo.
Kikosi
cha uokoaji kwa kutumia Helkopita kikiwa katika Hifadhi ya taifa ya
Mlia Kilimanjaro kwa ajili ya kutoa msaada kwa wageni .
Ndege
aina ya Helkopta inayotumiwa na Shirika la Kilimanjaro SAR katika
kufanya shughuli za uokoaji katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro.
Na Dixon Busagaga wa globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.SHIRIKA la Kilimanjaro SAR linayojishughulisha na utoaji wa
huduma ya utafutaji na uokoaji wa watalii wanaopata matatizo ya kiafya katika maeneo
yenye muinuko ikiwemo Mlima Kilimanjaro limetangaza kutoa bure huduma zake kwa waongoza watalii pamoja na wapagazi .
Hatua hiyo imefikiwa baada ya baadhi ya watu wanaojishughulisha na shughuli
za kusaidia wageni katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro kupata matatizo
ya kiafya na kushindwa kupata huduma huku kundi kubwa la watu hao kukosa Bima za Afya ,wengine wakikosa kabisa kipato
cha uhakika.
Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Kilimajaro SAR,Ivan Brown
alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya shughuli
zilizofanywa na kampuni hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanza
operesheni za uokoaji kwa kutumia njia ya Helkopta.
“Sisi ni wa kwanza na pekee katika Dunia hii tunaotoa huduma
ya uokoaji Bure kwa wote wanaofanya shughuli za mlima ,tunafahamu Wapagazi,Waongoza
watalii hawana bima, hawana njia zozote za kujipatia kipato ambazo zingesaidia
katika uokoaji”alisema Brown .
“Watakaopata matatizo ya kiafya au ajali wawapo mlimani wanaweza kuwasiliana nasi ,tutaaenda
juu na kumuokoa bila ya gharama zozote kwa sababu mipango yetu ni kuokoa maisha
,ndio sababu tunasema kwa waongoza watalii au wapagazi , uhai ndio kipaumbele
cha kwanza”aliongeza Brown .
Alisema shirika hilo likiwa linaadhimisha mwaka mmoja wa
utoaji huduma katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro tayari imetoa matibabu kwa zaidi
ya watu 250 huku akieleza kuweka rekodi ya kwanza Afrika kwa kumuokoa mgonjwa
aliyekuwa katika hali mbaya ,umbali wa Mita 5000.
“ Tayari tumetoa
huduma kwa zaidi ya wagonjwa 250 na miongoni mwao aliingia kwenye historia Afrika
ya kuwa mtu wa kwanza kuokolewa kwa na Helkopta katika eneo lenye urefu wa Mita
4800 ,katika kambi ya Cosovo Mlima Kilimanjaro June 22 mwaka jana”alisema
Borown .
“Tumeokoa waongoza watalii na
wapgazi 50 bila malipo ,bado tunashukuru kwa ushirikiano na msaada kutoka kwa taasisi mbalimbali kwa kuruhusu
mazingira kwa shirika letu kuweza kufanya shughulizaek za uokoaji maisha kwa
urahisi.
Mbali na shughuli ya utafutaji na uokoaji ,Kampuni yawapgazi 50 bila malipo ,bado tunashukuru kwa ushirikiano na msaada kutoka kwa taasisi mbalimbali kwa kuruhusu
mazingira kwa shirika letu kuweza kufanya shughulizaek za uokoaji maisha kwa
urahisi.
Kiliamanjaro SAR imeingia makubaliano na Hospitali ya St Joseph kwa kuanzisha
Kliniki ya kisasa “Kilimanjaro SAR High
Altitude Medicine Clinic” kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu kwa magonjwa
yatokanayo na muinuko .
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa shirika hilo ,Amour Abdalah
alisema kliniki hiyo ya kwanza Afrika imeanzishwa baada ya kubaini kwamba
mgonjwa anapookolewa kutoka mlimani anahitaji pia kupata huduma stahiki za matibabu
.
“Magonjwa ya mlimani yanahitaji ,matibabu maalumu ,na ndio
sababu tukaanza na operesheni ya kutoa huduma kwa kutumia Helkopta ikiwa ni
huduma ya kwanza kwa afrika na baadae mgonjwa huyu hufikishwa katika kliniki yetu
na kupatiwa matibabu”alisema Abdalah.
Alisema wazo la kuanzishwa huduma hizo lilianza mwaka 2013 baada ya kuona kwamba utoaji wa huduma sahihi
ya uokoaji na vifaa vya kitabibu vilihitajika na si pekee kwa Hifadhi ya Mlima
Kilimanjaro bali pia kwa Sekta ya Utalii Tanzania.
Abdalaha alisema kwa sasa kampuni ya Kilimanjaro SAR
imepanua wigo wa utoaji wa huduma za utafutaji na uokoaji katika maeneo mengine
zikiwemo hifadhi za taifa za Serengeti,Arusha,Manyara,Ruaha na Mikumi.
“Mlima Kilimanjaro umekuwa na wageni wengi wakifanya shughuli
za utalii ,na wengi wao baada ya kuapanda mlima Kilimanjaro wanaendelea na safari
nyingine kutizama vivutio vya utalii,jambo kubwa tunalofanya katika sekta ya
utalii ,tumewahakikishia usalama wageni wanaokuja Tanzania kupanda Mlima
Kilimanjaro “alisema Amour.
Katika kipindi cha mwaka mmoja Shirika la uokoaji ya
Kilimanjaro SAR tayari imejinyakulia tuzo tano za uongozi moja ikiwa ni ya
Tanzania ambazo ni “C.E.O of the Year 2018 Afrika “ ,“ H.R of the Year 2018 Afrika”
,“Dream Company to work for “ , “Employer Brand Afrika “ ,” Shirika Bora la kati Tanzania “ tuzo
iliyotolewa na ATE .
No comments :
Post a Comment