Friday, March 1, 2019

WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASSA AREJEA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM NA KUPOKEWA NA MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI


6
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akisalimiana kwa furaha na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia.
7 8
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akitangaza rasmi kurejea chama cha Mapinduzi CCM mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula, Katibu wa CCM Bashiru Ally, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamojan na Kada wa CCM Rostam Azizi.
9 10
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kumkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye amerejea rasmi CCM.
11-min
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo  katika mazungumzo na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, Kada wa CCM Rostam Azizi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally. PICHA NA IKULU

No comments :

Post a Comment