Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe.Jenista Mhagama akihutubia washiriki wa Warsha ya Mafunzo kuhusu
Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima
nchini Uganda kuja Tanga yaliyofanyika katika Ukumbi wa Tanga Beach
Resort Machi2, 2019.
Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Martine Shigela akihutubia wakati wa Warsha hiyo.
Sehemu ya Wajumbe walioshiriki
Warsha ya Mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani)
wakati wa warsha hiyo.
Sehemu ya Wajumbe walioshiriki Warsha ya Mafunzo hayo wakifuatilia hotuba uya mgeni rasmi wakati wa warsha hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Mhe.Jenista Mhagama akifuatilia jambo wakati wa warsha ya mafunzo hayo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya watendaji wa
Serikali wakati uzinduzi wa warsha hiyo mkoani Tanga.
Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’i Issa akizungumza jambo wakati
wa kikao cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na
baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Tanga alipokutana nao wakati wa Warsha ya
Mafunzo kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki
(EACOP) Machi 2, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Mhe.Jenista Mhagama (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na
washiriki kutoka Sekta ya Umma wakati wa warsha hiyo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
………………………………………
NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama leo Machi 2, 2019 amefungua warsha ya
mafunzo kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki
(EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda kuja Tanga, Tanzania.
Warsha hiyo iliwakutanisha zaidi
ya wadau 70 wakiwemo viongozi Waandamizi na Watendaji Wakuu wa Mkoa wa
Tanga, Wafanyabiashara wa mkoa huo pamoja na wanahabari na
kufanyika
katika ukumbi wa Tanga Beach Resort mkoani Tanga.
Akizungumza wakati wa kufungua
warsha hiyo ambayo itafanyika kwa muda wa siku mbili (Machi 02 na 03,
2019),Mhagama alisema Serikali inaendelea kuhimiza wananchi kutumia
fursa ya mradi huo katika kujiletea maendeleo yao nan chi kwa ujumla.
“Mkutano huu wa leo ni
matumaini kuwa, utaleta mageuzi makubwa ya mipango mikakati yetu ili
kuangalia fursa za ujio wa mradi huu kwa kuzingatia ni moja kati ya
mradi unaotarajiwa kuwa na manufaa mengi kwa nchi katika kuzalisha
ajira, kuendeleza urithishaji wa ujuzi na teknolojia pamoja na ubia kati
ya makapuni ya Tanzania na wageni,”alisema Mhagama
Waziri aliongezea kuwa, inawapasa
wananchi kutumia warsha hiyo kujadili na kuweka mikakati bora ya
kuzitumia fursa zitakazotokana na mradi kwa kuzingatia malengo mahususi
ikiwemo kujadili maendeleo ya mradi na fursa za ushiriki wa Watanzania
katika ujio ya mradi pamoja na kuwa na majadiliano kati ya Sekta Bonafsi
ya Umma ili kuchochea maendeleo endelevu ya kiuchumi
Aliongezea kuwa, mradi huo
utasaidia jamii kushiriki kikamilifu katika kujiletea maendeleo kwa
kuzingatia kuwa, ni zaidi ya robo tatu ya Bomba hili litapita Tanzania
na kuwanufaisha wananchi wake.
“Matarajio ni makubwa kwa
kuzingatia mradi huu unatarajiwa kupita katika mikoa 8 ikiwemo Kagera,
Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga ambapo
litapita katika Wilaya 24, Kata 134 na Vijiji zaidi 180 hivyo hatuna
budi kuchangamkia fursa kwa kuongeza jitihada za ongezeko la ushiriki
wetu,”alisistiza Mhagama
Naye Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Mhe.Martine Shiga aliendelea kuhimiza watendaji wake kushiriki
kikamilifu katika hatua zote za maandalizi kama Mkoa ili kuona namna
bora za kushiriki katika fursa hiyo kubwa ya kujileea maendeleo yao.
Naye Katibu Mtendaji, Baraza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa alieleza jitihada
za Baraza ikiwemo kuanzishwa kwa kanzi data ya nguvu kazi ambayo
inachukua takwimu za wafanyabiashara ili kiuwatambua kwa lengo la
kushirikisha katika program na kuona namba bora ya kuwashirikisha katika
fursa hizo.
“Niwaombe watanzania kuendelea
kujisajili katika kanzi data ya nguvu kazi ili tuweze kuwatambua, uwezo
na changamoto zenu na kuwashirikisha katika miradi mbalimbali ukiwemo
huu wa bomba la mafuta pamoja na kutatua changamoto hizo,” alisisitiza
Beng’i
AWALI
Warsha ya mafunzo hayo imeratibiwa
na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa ufadhili wa
Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) kupitia BEST Dialogue Tanzania kwa lengo
la kuwezesha viongozi na Wafanyabiashara wa Mkoa huo kufahamu maendeleo
na fursa zitakazotokana na mradi huo.Bomba hilo la Mafuta Ghafi la
Afrika Mashariki lina urefu wa KM 1,443 kati ya hizo KM 296 zipo nchini
Uganda na KM 1,147 zipo Tanzania
No comments :
Post a Comment