Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice
Tanzania Johnson Mshana (Kushoto) Akizungumza wakati wa droo ya tano ya
Promosheni ya Tia Kitu pata vituz, Kulia ni Afisa wa Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Jehud Ngolo. Promosheni hiyo ni ya muda wa wiki 8 ambapo
jumla ya washindi 120 watapatikana.
Mkuu wa Uhusiano MultiChoice
Tanzania Johnson Mshana (Wa pili kushoto) akiongoza droo ya kupata
washindi wa wiki ya 5 katika promosheni ya Tia kitu pata vituz ya DStv .
Kulia Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Jehud Ngolo ,
kushoto ni Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania akifuatiwa na Benson
Urio wa kitengo cha Teknohama cha DStv. Promosheni hiyo ni kwa wateja
wanaolipia kwa wakati kabla vifurushi vyao havijakatika hivyo kupata
fursa ya kushinda kifurushi cha miezi miwili. Promosheni hiyo ni ya muda
wa wiki 8 ambapo jumla ya washindi 120 watapatikana.
……………….
Dar es Salaam Machi 28, 2019.
Kampuni ya inayoongoza kwa huduma bora za vinga’muzi nchini, DStv
imetangaza washindi 15 wa droo ya 5 ya Promosheni hiyo ya wiki nane
inayoendelea nchi nzima maarufu kama “ Tia Kitu pata vituz”.
Promosheni hiyo ni ya wazi kwa
wateja wote wa DStv ambao watalipia vifurushi vyao kabla
havijakatika.
“Mteja yeyote wa DStv atakayelipia kifurushi chake kabla hakijakatika
moja kwa moja anaingia katika droo na fursa ya kujishindia kifurushi
chake kwa muda wa miezi miwili.” Alieleza Mkuu wa Uhusiano MultiChoice
Tanzania Johnson Mshana wakati akiendesha droo ya wiki ya nne ya
promosheni hiyo.
Akizungumza baada ya kufahamishwa
juu ya ushindi wake huo Bw. Yohana Francis ambaye ni mteja wa DStv
aliyepo mkoani Mbeya alisema kuwa amefurahi sana kuibuka mshindi na
kuongeza kuwa anaishukuru sana DStv na kuwaasa kuwa waendelea kuwajali
wateja wake hivyo hivyo.
No comments :
Post a Comment