Naibu Katibu Mkuu –Afya, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt. Dorothy
Gwajima akikagua ramani ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chamwino
wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utendaji kazi wa vituo vya afya vya
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino leo Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu –Afya, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt. Dorothy
Gwajima akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chamwino iliyopo
katika Kijiji cha Mlowa Barabarani wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua
utendaji kazi wa vituo vya afya vya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
leo Jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu –Afya, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt. Dorothy
Gwajima akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chamwino iliyopo
katika Kijiji cha Mlowa Barabarani wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua
utendaji kazi wa vituo vya afya vya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
leo Jijini Dodoma
Wananchi wa Mlowa Barabarani
wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu –Afya, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt. Dorothy Gwajima wakati akiongea
na wananchi hao wkatika ziara ya kikazi ya kukagua utendaji kazi wa
vituo vya afya vya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino leo Jijini Dodoma
………………………..
Na Majid Abdulkarim.
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Chamwino, katika kijiji cha Mlowa Barabarani wametakiwa kutoa
ushirikikiano katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo ili kuleta
maendeleo na kupunguza changamoto za afya nchini.
Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu
Mkuu Afya kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI), Dkt.Dorothy Gwajima wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua
utendaji kazi wa vituo vya afya vya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Jijini Dodoma.
Dkt. Gwajima amesema kuwa Serikali
pekee haiwezi kufanikiwa katika kuleta maendeleo bila kuwepo
ushirikiano kutoka kwa wananchi wake hivyo ni vyema wananchi
wakashirikishwa kikamilifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo
nchini.
Amesema Serikali imejenga
miundombinu ya afya nchini ikiwa na lengo la kuhakikisha huduma za afya
zinaboreka kuanzia ngazi ya Zahanati, Vituo vya afya, Hospitali za Mikoa
ili kupunguza changamoto katika sekta ya afya.
Akiendelea kufafanua amesema kuwa
wananchi wanatakiwa kuwa na dhamira ya dhati ya kusimamia miradi ya
ujenzi wa Hospitali za Wilaya ili zijengwe kwa ubora kulingana na fedha
zilizotolewa na Serikali.
“Wananchi hakikisheni mnasiamia
ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chamwino kwa umakini mkubwa kwa
kuangalia gharama zinazotumika zinaenda sambamba na majengo yanayojengwa
kwa kuwa Hospitali hizi ni mali ya wananchi” Amesisistiza Gwajima
Akifafanua kuhusu ubora wa huduma
zinazotolewa kwenye vituo vya afya amesema Serikali imejenga miudombinu
ya afya nchini lakini bado changamoto kubwa ni watendaji waliopo katika
vituo hivyo kutotimiza majukumu yao kwa uadilifu katika kutoa huduma
bora kwa jamii hali ambayo inasababisha wananchi wengi kutokufika katika
vituo hivyo.
“ Baadhi ya watoa huduma wamekuwa
na lugha chafu kwa wateja, kutokuwa na ukarimu, kutowajibika kikamilifu,
uzembe, rushwa ambapo vitu vyote hivi vinapelekea wananchi kutokuja
kutibiwa kwenye vituo vya afya vya Serikali na kukimbilia vituo binafsi,
naagiza watoa huduma wote nchini kuhakikisha wanafanyakazi kwa weledi
katika kuwahudumia wananchi” Amesema Gwajima
Aidha amewataka wananchi
kuhakikisha wanatoa taarifa pale wanapojibiwa vibaya na watoa huduma za
afya nchini na Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kinidhamu
watumishi wote watakaobainika kuwa na makosa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Chamwino, Athuman Masasi amesema kuwa watahakikisha
wanakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo kwa wakati ili wananchi
waanze kupata huduma.
No comments :
Post a Comment