Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa
Prof. Palamagamba J. Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Mikhail Bogdanov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Urusi katika Ofisi Ndogo ya Wizara Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Waheshimiwa Mawaziri
wamezungumzia masuala mbalimbali yaliyolenga kuboresha na kuimarisha
uhusiano na ushirikiano baina ya mataifa haya mawili, hususan, katika Nyanja ya kidiplomasia, nishati, biashara na uwekezaji. Naibu Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. |
Waheshimiwa
Mawaziri wanaendelea na mazungumzo hayo, huku ujumbe aliofuatana nao
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi ukifuatilia mazungumzo hayo
|
No comments :
Post a Comment