Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akimsikiliza Bw. Nicolas Agostini kutoka
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya “Defend Defenders alipokutana na viongozi
hao Mjini Geneva nchini Uswisi Februari 28, 2019
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Prof. Palamagamba Kabudi na ujumbe wake wakiwasikiliza viongozi wa
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya “Defend Defenders alipokutana na
viongozi hao Mjini Geneva nchini Uswisi Februari 28, 2019
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.
Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) na ujumbe wake katika picha ya pamoja na
Viongozi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya “Defend Defenders” Bw. Hassan
Shire (Mkurugenzi Mtendaji mwenye tai Nyeusi) na Bw. Nicolas Agostini
(Mwakilishi mwenye tai nyekundu) kwenye Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania
Umoja wa Mataifa baada ya kumaliza mazungumzo yao Mjini Geneva nchini
Uswisi Februari 28, 2019
…………………………
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.
Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) amekutana na kufanya
mazungumzo na
Viongozi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya “Defend Defenders” Bw. Hassan Shire na Bw. Nicolas Agostini.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika
Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Geneva nchini
Uswisi wakati wa Kikao cha 40 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa
Mataifa kinachofanyika Mjini Geneva ambacho Prof. Kabudi anahudhuria.
Prof. Kabudi na viongozi wa
Taasisi hiyo wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu haki za binadamu
nchini ambapo pia walimkabidhi Prof. Kabudi Ripoti yao ya mwaka 2018
ambayo iliishutumu Serikali kwa ukiukwaji wa masuala mbalimbali ya haki
za binadamu.
Akizungumza na viongozi hao, Prof.
Kabudi alieleza masikitiko yake kwa Taasisi hiyo na Taasisi nyingine
kwa kuishutumu Serikali na kutoa ripoti na taarifa mbalimbali ambazo
zinatoa shutuma dhidi ya Serikali bila kuwasiliana na Serikali ili
kupata ufafanuzi wa shutuma hizo.
Alisema vitendo hivyo
vinasababisha upotoshaji mkubwa wa hali halisi ya masuala ya haki za
binadamu nchini na jitihada za Serikali katika kutekeleza wajibu wake wa
kukuza, kulinda na kuheshimu haki za binadamu.
Prof. Kabudi alisisitiza umuhimu
wa taasisi hiyo na taasisi mbalimbali kuishirikisha Serikali ili kupata
maelezo kutoka pande zote na kupata uelewa wa jambo kabla ya kutoa
taarifa zao ambazo zinaishutumu Serikali.
Amesema Tanzania kama nchi
nyingine inapata changamoto mbalimbali wakati inatekeleza jukumu yake la
kulinda, kuheshimu na kukuza haki za binadamu nchini na pale
inapoonekana kuwa haitekelezi ipasavyo wajibu iliyonao ni vizuri
mashauriano yakafanyika na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha
utekelezaji wa wajibu wa kulinda na kustawisha haki za binadamu kwani
mawasiliano yangefanyika ripoti hiyo isingetoka hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ya “Defend Defenders”
alikiri kuwa hawakuwasiliana na Serikali kabla ya kutoa ripoti hiyo, na
alimshukuru Prof. Kabudi kwa kuridhia kukutana nao na kwamba Taasisi
hiyo imepokea ushauri ya Mhe. Waziri na kuahidi kuendelea kujadiliana na
Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria ambayo inasimamia masuala
ya haki za binadamu.
Waziri Kabudi alitumia fursa hiyo
kuukaribisha uongozi wa Taasisi hiyo Tanzania ili wapate ufafanuzi wa
masuala mbalimbali ambayo yameripotiwa kuhusu Tanzania na kama ina maoni
au mapendekezo kuhusu namna bora ya kuboresha haki za binadamu nchini
wanakaribishwa kujadiliana na Serikali kupitia Wizara ya Katiba na
Sheria.
No comments :
Post a Comment