Monday, March 11, 2019

KCB BANK TANZANIA BIASHARA CLUB YAFANYA SEMINA ARUSHA


Pic001
Bi. Christine Manyeye,Mkuu wa Idara ya Masoko na Mahusaino akijibu maswali kutoka kwa wafanya biashara wa jijini Arusha katika warsha ya Biashara Club iliyofanyika Mt. Meru Hotel tarehe 05 Machi 2019. Semina hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 iliwajumuiasha wadau mbali mbali katoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.
Pic002
Nd. Ernest Jackinda, Afisa Masoko wa TANAPA akiongea na wageni waalikwa katika warsha ya Biashara Club iliyofanyika Mt. Meru Hotel tarehe 05 Machi 2019. Semina hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 iliwajumuiasha wadau mbali mbali katoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.
Pic003
Nd. Masika Mukule, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Masuala ya Kibenki akiongea na wageni waalikwa wakati wa maongezi ya ana kwa ana katika warsha ya Biashara Club iliyofanyika Mt. Meru Hotel tarehe 05 Machi 2019. Semina hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 250 iliwajumuiasha wadau mbali mbali katoka sekta ya utalii wakiwemo Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.
…………………………………………………………………………………
Benki ya KCB Tanzania imefanya kongamano la kwanza ya Biashara Club kwa mwaka 2019 jijini Arusha baada ya kuandaa kongamano kama hilo jijini Mwanza mwishoni kwa mwaka 2018. Zaidi ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria za kodi, KCB Biashara Club pia inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara zao kwa kuwakutanisha na wafanyabiashara wa nje na ndani ya nchi. Tangu kuzinduliwa kwake, KCB Biashara Club imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara katika seckta ya SME kwa kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati yaani (SME) pamoja na kuwaonyesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli zao za kibiashara.
Biashara Club kwa jijini Arusha lilifanyika Mt. Meru Hotel tarehe 05 Machi 2019 na lilikuwa na lengo mahususi la kukutanisha wadau mbali mbali katika sekta ya utalii wakiwemo wafanyabiashara. Kongamano hilo lilifanyika katika sehemu mbili ambapo sehemu yakwanza ilikuwa mahususi kwa wateja wa Benki ya KCB wapatao 250, huku sehemu ya pili ikiwa ni jukwaa la wazi kwa wakazi wengine wa Arusha kupata elimu ya huduma za kibenki kutoka kwa wataalam wa Benki ya KCB.
Akiongea wakati wa kufungua semina hiyo, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Bi. Christine Manyenye alisema Benki ya KCB imefanya juhudi za mahususi za kuwaleta wadau kama Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Tanzania Revenue Authority (TRA), Tanzania Association of Tour Operators (TATO) and East Africa Business Council (EABC) kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.
Kwa upande wake Meneja wa Tawi, KCB Bank Arusha, Bi. Judith Lubuva aliwapongeza wafanya biashara, wadau na wakazi wa Arusha kwa kuhudhuria kongamano. Aliongeza kwamba kongamano hilo limefanyika kwa wakati muafaka ambapo sekta ya utalii inaendelea kuimarika katika kanda ya kaskazini na Tanzania kwa ujumla.
Nd. Abdul Juma, Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabishara Wadogo na wa Kati (SME) aligusia fursa tofauti zinazoletwa na Biashara Club zikiwemo kuwakutanisha wafanya biashara mbali mbali wa nje na ndani ya nchi, kupanua wigo wa masoko kupitia safari za pamoja kwenda nchi kama China, Malaysia na Afrika Kusini. Nd. Juma aliwahakikishia wadau kwamba KCB Bank ina dhamira ya kuinua sekta ya utalii kwa kuitambulisha Tour Operator Account inayowezesha malipo ya kieletroniki pamoja na kuwana faida zingine zikiwemo huduma kwa njia ya mtandao kuwa bure na kutoa pesa bure.
Akiongea katika warsha hiyo, mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA), Mr. Ombeni Urio aliyekuwa mshauri wa masuala ya kodi, alisisitiza umuhimu wa wafanya biashara hao kufuata kanuni za kodi. Aliipongeza Benki ya KCB kwa kumualika ili aweze kutoa elimu hiyo ambayo ilikuwa inahitajika kwa sana.

No comments :

Post a Comment