Friday, March 1, 2019

JAJI MKUU ATAKA MASHAURI YA MIRATHI KUMALIZIKA KWA WAKATI

FC4A0024-min
JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA AKISALIMIANA NA WATUMISHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MTWARA MARA BAADA YA KUWASILI KUANZA ZIARA KATIKA MKOA WA MTWARA KWA AJILI YA KUKAGUA SHUGHULI ZA MAHAKAMA
FC4A0037-min
JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA AKISAINI KITABU CHA WAGENI OFISINI KWA MKUU WA MKOA WA MTWARA MHE. GELASIUS BYAKANWA ALIPOMTEMBELEA OFISINI KWAKE IKIWA NI SEHEMU YA ZIARA YAKE
FC4A0048-min
JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA AKIMKABIDHI MKUU WA MKOA WA MTWARA  VITABUI VINAVYOHUSU MAADILI
FC4A0097-min
JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA AKIMKABIDHI MKUU WA WILAYA YA TANDAHIMBA MHE. SEBASTIAN WARYUBA KITABU KINACHOELEZEA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA MAHAKAMA YA TANZANIA PAMPOJA NA KITABU CHA MAADLI.
 
Lydia Churi Ntambi
…………………………..
Lydia Churi-Mahakama, Mtwara
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameagiza kupelekewa mashauri yote ya Mirathi nchi nzima ili aweze kujua ni changamoto gani inayofanya yachelewe kumalizika na
kupanga mkakati wa kisheria ili mashauri hayo yawe yanaisha ndani ya muda uliowekwa kisheria.
Akizungumza katika ziara yake ya kikazi aliyoanza leo mkoani Mtwara, Jaji Mkuu alisema katika mahakama za Mwanzo mashauri hayo yanatakiwa uisha ndani ya miezi sita lakini yapo mengine yamekaa zaidi ya miaka kumi.
Alisema kutokana na kuchelewa kumalizika kwa mashauri haya, wakati mwingine humfanya msimamizi wa mirathi kuendelea kunufaika na mali za marehemu wakati warithi wapo na wanataabika kwa muda mrefu.
Jaji Mkuu amesema ametoa agizo hilo pia kwa kuwa mashauri ya aina hiyo huweza kuzalisha migogoro mingi katika jamii na kusababisha haki kutokupatikana kwa wakati.
Akizungumzia changamoto nyingine zinazoikabili Mahakama ya Tanzania katika kutekeleza jukumu lake la msingi la utoaji wa haki, Prof. Juma alisema Mahakama inakabiliwa na changamoto kubwa ya wananchi kutofahamu taratibu za kisheria jambo linalosababisha washindwe kupata haki kwa wakati.
Alisema hivi sasa Mahakama ya Tanzania imejiwekea utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya taratibu za kisheria kabla ya kesi kuanza kusikilizwa Mahakamani ili kuwasaidia wanannchi kutambua nini cha kufanya
Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama imeamua kuwa wazi katika kutekeleza majukumu yake ikiwa ni moja ya hatua muhimu za mapambano dhidi ya rushwa ndani ya Mhimili huo.
Awali akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa, Jaji Mkuu aliwaomba wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini kushirikiana na Mahakama ya Tanzania katika kuwaelimisha wananchi taratibu za mchakato wa upatikanaji wa haki.   
Alisema Mahakama inachangia utulivu na Amani katika nchi pale inapotekeleza jukumu lake la msingi la utoaji wa haki kwa wakati na endepo Mahakama haitafanya kazi yake vizuri ni wazi itatoweka. Aliongeza kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 pia imetoa mwelekeo wa Amani.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akimkaribisha Jaji Mkuu Ofisini kwake alisema Serikali kupitia Mkoa wake inashirikiana vizuri na Mahakama katika kuwahudumia wananchi na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.
Wakati huo huo, Mtendaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Bwn. Solanus Nyimbi ili kutatua changamoto ya uchakavu na ukosefu wa miundombinu ya Mahakama hususan majengo, Mhimili huo umeandaa Mpango Kabambe wa ujenzi uliozingatia maeneo yanayotakiwa kujengwa majengo mapya ya Mahakama, pamoja na yanayotakiwa kufanyiwa ukarabati mkubwa.
Alisema hivi sasa majengo yanayoendelea kujengwa ni pamoja na Mahakama za Mwanzo 22, Mahakama za Wilaya 20, Mahakama za Mikoa (Hakimu Mkazi) 8 pamoja na Mahakama kuu 2, zinazojengwa katika mikoa ya Mara na Kigoma.
Alisema wilaya ya Tandahimba nayo iko kwenye mpango wa kupatiwa jengo litakalojumuisha mahakama ya Wilaya pamoja na Mahakama moja ya Mwanzo. Aliongeza kuwa lengo ni kuwa na Mahakama katika kila makao makuu ya Tarafa.
Bwn. Nyimbi alisema ifikapo mwaka 2021 wilaya zote zisizo na majengo ya Mahakama zitakuwa tayari zimepatiwa majengo hayo ambapo ujenzi huo utatumia fedda za ndani pamoja na za Benki ya Dunia.
Jaji Mkuu anaendelea na ziara yake ya kikazi aliyoianza leo katika mkoa wa Mtwara. Alitembelea Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara pamoja na Mahakama ya wilaya ya Tandahimba ambapo pia alipata fursa ya kuzungumza na watumishi.

No comments :

Post a Comment