WAZIRI wa Maji Proffesa Makame
Mbarawa akizungumza mara baada ya kutembelea wilaya ya Kilindi wakati wa
ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda Mtondoo
Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua akimueleza changamoto ya maji ya wilaya hiyo Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa wakati alipofanya ziara wilayani humo |
MKUU wa wilaya ya Kilindi Sauda Mtondoo akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa |
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame
Mbarawa kulia akitoka eneo la mradi mara baada ya kulikagua wakati wa
ziara yake wilayani Kilindi kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda
Mtondoo
WAZIRI wa
Maji Proffesa Makame Mbarawa amempa muda wa siku nne Mkandarasi wa Kampuni ya
Sajo Octavious Nduke kuhakikisha mradi wa maji wa Bokwa uliopo eneo la Mabobwe
wilayani Kilindi unakamilika na wananchi
waweze kunufaika na huduma ya maji ndani ya wakati huo.

Mradi huo ambao umegharimu zaidi ya sh.milioni
300 ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2017 na ulitakiwa kukamilika mwaka jana ili
kuweza kutoa maji na kuondoslkha kero kwa wananchi hao hata hivyo baadae maji
hayakuweza kulikotokana na changamoto mbalimbali.

Alisema hayo mara baada ya kuutembelea
na kuzungumza na wananchi ambapo alisema iwapo mkandarasi huyo atashindwa
kufanya kazi hiyo kwa kipindi hicho ambacho amemwaagiza yeye anajua wapi atakwenda
kuchukua fedha ili waweze kuwanunuliwa mota ambayo itafungwa ili wananchi
waweze kupata huduma ya maji ili kuondokana na kero zilizopo

“Lakini pia nikuambie kama hautanunua
mota hii wala usisubutu kuomba kazi nyengine kwa sababu utakuwa umetutapeli ….hauwezi
kuendelea kula fedha wakati wananchi wanaendelea kuteseka hii haikubaliki akifanya
ujuaji mimi najua mahali pa kwenda kuchukua fedha tuna fedha yake tumeizuia
akifanya kupindisha tunachukua hela tunanunua mota muweza kupata maji “Alisema
Waziri Mbarawa.

“Nendeni mpaka Ijumaa mhakikishe mmekwisha
kununua mota na kuifunga hapa wananchi waweze kupata huduma ya maji kutokana na
kwamba mradi huu ulikuwa kwenye muda wa matazamia hivyo ikitokea chochote
kimeharibika kwenye miundombinu hii ndani ya mwaka mzima atalazimika
kutengeneza kwa fedha zake za mfukoni na ndio maana ya muda wa
matazamia”Alisema

Awali akitoa taarifa za mradi huo
wakati wa ziara hiyo, Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya Sajo, Octavious
Nduke alisema mradi huo tayari ulishakamilika kwa asilimia mia moja na wananchi
wakaanza kupata maji lakini baadae ikajitokeza changamoto ya kuungua kwa vifaa.

“Mh Waziri katika mradi huu maji
yalikuwa yanatokana na wananchi kuweza kuyapata lakini kuna changamoto ya
kuungua baadhi ya vifaa na hivyo kupelekea kukwama kuendelea kutoa maji lakini
tutalifanyia kazi “Alisema

Akijibu changamoto hiyo Waziri Profesa
Mbarawa alisema suala la kununua vifaa vilivyoungua ni jukumu la mkandarasi
hivyo kumtaka afanye hivyo mara moja ili kuwaondolea wananchi adha
wanazokumbana nazo.

Naye kwa upande wake Diwani wa kata ya
Bokwa Idirisa Mgaza alimueleza Waziri huyo kwamba mradi huo umewapa shida kama
viongozi huku wananchi wao wakiendelea wanataabika juu ya suala la
upatikanaji wa maji.

“Mh Waziri tunaomba tatizo hili uone
namna ya kulipatia ufumbuzi kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa eneo hilo
wanaonekana na changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji “Alisema.

Katika hatua nyingine Mbunge wa jimbo
la Kilindi Omari Kigua amemuomba waziri Mbarawa kuwapelekea fedha kwa ajili ya
mradi mkubwa wa maji ambao utakuwa mkombozi wa changamoto ya maji kwenye wilaya
hiyo ambapo waziri ameahidi kulifanyia kazi.

Alimueleza
waziri huyo kwamba suluhu ya ufumbuzi wa changamoto ya maji wilayani humo ni mradi
mkubwa wa maji kutoka Mto mkubwa Pangani au Ruvu Korogwe yafika hadi makao
makao makuu ya wilaya yatasaodoa kuondokana na adha wanayoipata kwa sasa.

“Lakini
maji hayo yatakapofika makao makuu ya wilaya yanaweza kufika kwen ye vijiji mbalimbali kwa urahisi na
hivyo wananchi kuweza ,kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa maisha ya kila siku
“Alisema

No comments :
Post a Comment