Jane Mihanji mmoja wa wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya TAWA walioteuliwa
……………………………………………….
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (Mb.), amekamilisha uteuzi wa safu ya
wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori
Tanzania – (TAWA), kulingana na mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu
cha 3.1.1 cha amri ya uanzishwaji wa Mamlaka ya TAWA ( GN na. 135 ya
mwaka 2014) kwa kuwateua wajumbe wengine wawili.
Wajumbe walioteuliwa kukamilisha safu inayotakiwa ni;
- Jane Claude Mihanji na
- Bi Magdalena Joseph Kimaty
Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 26 Oktoba, 2018.
Wakati huo huo, Waziri wa Maliasili na Utalii, amebatilisha uteuzi wa Dkt. Freddy S. Manongi kuwa mjumbe wa bodi ya TAWA.
Imetolewa na
Dorina G. Makaya
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
27 Februari, 2019
No comments :
Post a Comment