Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza nchini, Phaustine Kasike akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya NBC, Theobald Sabi(kushoto) alipotembelea ofinisi za Makao
Makuu ya Magereza jijini Dar es salaam, leo Februari 25, 2019.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza nchini, Phaustine Kasike akizungumza katika kikao na uongozi
wa Benki ya NBC, uliomtembelea ofinisi kwake, Makao Makuu ya Magereza
jijini Dar es Salaam Februari 25, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
NBC, Theobald Sabi(kushoto) akizungumza na Kamishna Jenerali wa Jeshi
la Magereza nchini, Phaustine Kasike alipokutananaye kwa mazungumzo juu
ya kuangalia njia bora za kudumisha uhusiano baina ya Benki ya NBC na
Jeshi la Magereza nchini, katika Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es
Salaam, Februari 25, 2019. Wengine kulia ni Maafisa Waandamizi wa Bendi
hiyo.
Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama(kulia) pamoja na Kamishna wa
Huduma za Urekebishaji, Mhandisi, Tusekile Mwaisabila9kushoto)
wakifuatilia mazungumzo hayo katika Ofisi ya Kamishna Jenerali wa
Magereza nchini.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini,
Phaustine Kasike(wa tatu toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi(wa tatu toka kushoto)
pamoja na Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza na Benki ya NBC
katika Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es Salaam, Februari 25, 2019(Picha na Jeshi la Magereza).
Na Lucas Mboje, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya
NBC,Theobald Sabi leo amekutana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Phaustine Kasike na kufanya mazungumzo yaenye lengo la kuangalia njia
bora zaidi za kudumisha na kuboresha uhusiano baina ya pande zote
mbili.
Akizungumza katika mkutano huo
ambao pia ulijumuisha maafisa waandamizi kutoka Benki ya NBC na Jeshi
la Magereza, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi
alilishukuru Jeshi hilo kwa kuwa mdau mkubwa wa Benki kupitia mikopo,
akaunti za mishahara za askari na pamoja na Shirika Magereza ambayo kwa
muda mrefu imekuwa ikitoa huduma kwa askari wa Jeshi hilo.
“Nichukue fursa hii kulishukuru
Jeshi la Magereza kwa mahusiano ya kibiashara ambayo limekuwa
likitupatia, nilipongeze Shirika la Magereza kwa kuendelea, kuwa mdau
muhimu katika huduma zetu za kibenki pamoja na Maafisa na askari wa
Jeshi la Magereza”. Alisema Mkurugenzi Sabi.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la
Magereza nchini, Phaustine Kasike alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya NBC, Theobald Sabi kwa kutembelea Jeshi hilo na kuipongeza
Benki ya NBC kwa maboresho mbalimbali katika huduma zake za kibenki.
Jenerali Kasike amesema kuwa
Jeshi la Magereza litaendelea kushirikiana na Benki ya NBC katika miradi
yake ya kiuwekezaji na huduma mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa Jeshi
hilo.
“Nikuombe Mkurugenzi Sabi na
uongozi mzima wa Benki ya NBC kuona uwezekano wa kusaidiana katika
huduma mbalimbali za kijamii magerezani kwani Jeshi la Magereza ni watoa
huduma kwa jamii hususani huduma ya urekebishaji wa wahalifu ambao ni
zao la jamii yenyewe”. Alisema Jenerali Kasike.





No comments :
Post a Comment