Wakili wa Serikali katika Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Obadia Kajungu akitoa maelezo kuhusu
majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa Mkemia Mkuu wa
Serikali Dr. Fidelice Mafuniko ( aliyevaa koti)wakati alipofika kwenye
Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mkemia Mkuu alifuatana
na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Jinai na Huduma za
Vinasaba Bw. David Elias
Watoto hawa walikuwa sehemu ya
wananchi waliotembelea Banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali. kutoka
kushoto Christina, Christian ( darasa la 11 A) Catherine Mutambuzi (
darasa la 11A), Proscovia Christian ( darasa la V1B) na Prisca Christian
(111A) wanaosoma shule la St. Ignatius ya Jijini Dodoma walimuuliza
maswali mbalimbali Wakili wa Serikali Anna Mkongwa ambaye aliwajibu wa
ufasaha maswali yao .
Mwakilishi wa Mkazi wa Bank ya
Dunia nchini Tanzania B.i Bella Bird akipata maelezo kutoka kwa Wakili
wa Serikali Obadia Kajungu kuhusu Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali wakati Bi Bird alipotembelea Banda la Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Maonesho ya wiki ya sheria
yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square Dodoma wengine katika
picha ni wanafunzi Godliver Adrian ( Msalato) na Auxarus Chambulila (
Mzumbe) ambao wamepangiwa Banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama
sehemu ya mafunzo yao. Wanafunzi hawa na wengine waliotembelea Banda
hili wameonyesha nia yao ya kuwa wanasheria.
Picha na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
……………………..
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kati ya Taasisi inayoshiriki maonesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea katika Viwanja vya Nyerere ‘Suare’ Jijini Dodoma. Wananchi mbalimbali wa rika tofauti wamefika katika Banda hili wakiwa na shinda mbalimbali au kupatiwa elimu kuhusu utendaji na majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mbali ya Wananchi wapo viongozi ambao wamefika katika Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Viongozi hao ni pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali Dr. Fidelice Mafumiko.
No comments :
Post a Comment