Thursday, January 31, 2019

VIKWAZO VISIVYO RASMI KATIKA BIASHARA BADO NI CHANGAMOTO NCHI ZA EAC


IMG_20190131_172109-min
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Vikwazo visivyo rasmi Usalama utekelezaji wake bado ni changamoto ya kufikia malengo ya kibiashara kwenye nchi za ukanda wa Afrika mashariki katika sekta ya biashara ambapo baraza la biashara limewataka viongozi wa jumuiya hiyo kulingalia na kuchukuwa hatua za maksudi kulitolea tamko.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa Ofisi za Baraza la biashara Afrika mashariki(EABC) jijini hapa Mwenyekiti wa baraza la mawaziri kwenye jumuiya hiyo amesema suala hilo ni miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa na wakuu wa jumuiya hiyo kesho jijini hapa watakapokutana
ili kuondoa changamoto hiyo.
Amesema kuwa changamoto ya vikwazo vya kiusalama na mtangamano wa kibiashara bado umekuwa changamoto kwenye Boda zetu na kuwafanya wafanyabiashara kutoenda na muda hivyo kuchelewesha maendeleo tunatarajia wakuu wan chi zetu watalijadili ili kuwezesha kuondoa changamoto hizo.
“Kama unafanya biashara hakuna usalama wa uhakika basi hapo hakuna uhakika hivyo tumeliona tumeliona hilo na miongoni mwa mambo tulioweka kujadiliwa ni hilo la usalama na vikwazo visivyo rasmi katika biashara kuondolewa na kupatiwa ufumbuzi”alisema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo la biashara kwenye Jumuiya ya Afrika mashariki Nick Nesbitt amesema kwa miongo miwili baraza hilo limepiga hatua kubwa kuelekea kwenye nchi hizo kuwa na nguvu ya kiuchumi kutokana na fursa nzuri za kibiashara na kuwataka wakuu kuona umuhimu wa kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika nchi hizo
Ameeleza kuwa vikwazo visivyo rasmi ni moja ya changamoto kubwa ya kufikia malengo ya kukuza biashara katika ukanda wetu kwani ukuaji wake umekuwa bado hauendani na ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara(SADC) hivyo mikakati inahitajika kufikia japo asilimia 40
Nae Mkurugenzi wa Baraza hilo la biashara Afrika mashariki  ameeleza mafanikio na changamoto mbali mbali zinazolikabili baraza hilo kwa miongo miwili kuwa ni changamoto za kiusalama na vikwazo visivyo rasmi kwa wafanyabiashara wanavyokumbana navyo kuelekea kwenye mtangamano wa kibiashara.
Amesema kuna mafanikio mengi yamepatikana ndani ya miaka hii 20 ya uwepo wa EABC na kuwashukuru wakuu kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya kibiashara katika muingiliano wan chi moja kwenda nyingine
Kwa upande wake mwenyekiti wa Baraza la wafanyabiashara nchini Tanzania Samuel Nyanchae amesema kuwa vikwazo visivyo kodi bado ni changamoto kubwa kwa wafanyabiashara wa nchi hizo na kuwataka wakuu hao kuendelea kuona njia nzuri ya kuhuisha maazimio yake kufikia malengo tarajiwa.
“Naona maadamu vimetakiwa viondolewe naomba utekelezaji wake ukazingatiwa ili kuondoa changamoto yake kwa wana biashara wan chi zetu kwani kuna baadhi ya nchi zetu bado wapo chini katika utekelezaji wa vikwazo hivyo visivyo rasmi”alisisitiza Nyanchae

No comments :

Post a Comment