Thursday, January 31, 2019

SHERIA YA KWANZA INAYOTUNGWA KWA KUWAFUATA WADAU WATOE MAONI YAO


4
Hii ni rasimu ya sheria ya kuigwa inayotungwa kwa kushirikisha wadau kwa kuwafuata walipo watoe maoni yao yatakayosaidia kuboresha sheria ya Uvuvi na ile ya ukuzaji viumbe maji.
 Haya yalibainishwa leo mkoani Mara na mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt.Vicent Nano,wakati1 akifungua kikao cha siku moja cha wadau wa Uvuvi kolichokuwa na lengo la Wadau hao kutoa maoni yao katika Rasimu ya Sheria za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji.
 Mkuu huyo wa wailaya alisema kuwa,rasimj hii Sheria ya Uvuvu na Ukuzaji viumbe maji itakuwa ni ya kwanza kiutaratibu kwa kuwafuata wadau walipo watoe maoni yao.
 Aliendelea kusema kuwa,rasimu yaSheria hizi zitakapokamilika zitawalinda wadau wa Uvuvi na raslimali za uvuvi.
2
Aidha liendelea kuwa Rasimu hizi zimekuja kwa wakati muafaka kwa vile sekta inakabiliwa na changamoto nyingi,hivyo wadau watatoa maoni yao ambayo yatasaidi kuiboresha.
 Vilevile Dkt.Nano aliwaasa wadau hao kuwa mnapofikiria masuala ya Uvuvi na Ukuzaji viumbe maji wanatakiwa kuzingatia suala zima uendelevu wake pia.
 Aliendelea kuwaasa kuwa,Ziwa victoria tulione kama tuliazimwa na Mungu ilikujiimarisha kiuchumi wakati huo tukilinda raslimali hiyo kwa faida ya vizazi vijavyo.
3
Awali kaimu mkurugenzi wa Ukuzaji viumbe maji Dkt.Hamisi Nikuli aliwataka wadau hao kuzingatia umuhimu wa kikao hicho ilikutoa maoni yatakayo boresha rasimu hizi mbili ilikuondoa uonevu katika kutekelezaji wake wakti huo huo tuhakikishe kwamba raslimali za Uvuvi zina lindwa na kuwa endelevu.
Nawo wadau kwa nyakati tofauti wakitoa maoni yao walisema kuwa mkurugenzi wa Uvuvi amepewa madaraka makubwa sana ya kutunga sheria na kuweka adhabu ambazo zinakuwa ni kandamizi kwetu sisi,hivyo apunguziwe madaraka hayo.
index
Aidha wamesema leseni ya uvuvi moja itambulike nhini kote kama ilvyo leseni ya dereva wa gari inatambulika nchini kote,ilikuondoa usumbufu unaojitokeza kwa wadau wa Uvuvi.
Vilevile wamesema wanataka Mabondo ya samaki aina ya Sangara ya wekewe utaratibu ili biashara yake ifanyike kihalali na kisheria na hatimaye wavuvi wanufaike nayo.
Wakiendelea kutoa maoni ya walisema waruhusiwe kusafirisha mizigo midogo ya mazao ya samaki katika mabasi na vyombo vingine kama pikipiki,kwa kuwa mara nyingi mazao haya ni mboga tu ya kumia nyumbani.

No comments :

Post a Comment