HakiPensheni
Meneja
Mkuu wa Bima ya Maisha Sanlam, Wilson Mnzava (kulia), akikabidhiwa mkataba wa
Bima ya Elimu wa "Sanlam Education care" wakati wa uzinduzi wake siku za nyuma
Na
Christian Gaya, majira Ijumaa, Februari 01, 2019 www.majira.co.tz
Unafikiri kwa nini kuna
umuhimu mkubwa kwa kampuni za bima nchini, kuwekea maanani makubwa sana juu ya utoaji
wa huduma bora kwa wateja wao. Kwa sasa kampuni na taasisi nyingi zinaendeshwa
kwenye mazingira ya ushindani. mkubwa ambao kila siku unaongezeka. Na ushindani
huu ni wa kimataifa na wakati huo huo na masoko ulimwenguni... yanaendelea
kuongezeka kila siku.
Leo gharama za kumpata mteja
mpya mara nyingi zinazidi hata gharama za kumbakiza mteja wa siku nyingi. Mteja
aliyeridhika na huduma huwa habishani na bei za huduma au bidhaa unazotoza na
kwa maana hiyo kunakuwepo na shughuli au kazi ndogo sana za kufanya masoko na
za uuzaji za kumhudumia mteja wa namna hii kuliko utekelezaji au shughuli
ambazo ungefanya kwa kumtafuta mteja mpya.
Matokeo yake kwa sasa wakati
wa teknolojia na habari na mawasiliano shughuli za biashara zaidi humgusa
mteja. Kwa kuongezeka kwa ushindani bima nchini zinahitaji kuunganishwa na aina
zote za mitandao ili kuboresha mawasiliano na hatimaye kumridhisha mteja.
Makampuni ya bima lazima ziweke
malengo na mikakati ya rasilimali zao kwa nguvu zote kwa ajili ya kuwalenga na
kuwabakisha wateja bora na wanaovutia na kuhakikisha ya kuwa wanapanua msingi
wa wateja ambao wataleta faida kubwa ndani ya biashara ya bima hasa kwa
kuwakatia bima mbalimbali na kukusanya tozo itakayotunisha kampuni ya bima kwa
muda mrefu ili kutimiza ahadi za wateja wao wa muda mrefu na ya muda mfupi.
Faida kubwa kwa mteja kama
atapatiwa huduma bora anakuwa amezoea na huduma ya hali juu kwa kuridhika na
kiwango cha huduma na jinsi kampuni ya bima inavyomjali.
Matokeo yake ni kwamba mteja anakuwa
hana muda wa kuhangaika wa kutafuta kampuni nyingine ya bima wa kuhamia wa
kumpatia huduma bora zaidi hiyo anayopata. Gharama au bei ya huduma au
bidhaa siyo kwa kila kitu, mteja anabaki
kuwa mwaminifu wa kampuni ya bima inayomridhisha na huduma anazotaka hata kama
kutatokea na kampuni ya bima nyingine inayotoa huduma na bidhaa zinazofanana na
kwa bei au gharama za chini.
Na faida kubwa kwa kampuni kwa
kutoa huduma bora na hali ya juu ya kumjali mteja ni kwamba mteja aliyeridhika
mara nyingi ni mtu ambaye atabaki kuwa mteja wake. Na jinsi ya kumpata mteja
mpya kwa kawaida ni gharama za hali ya juu sana kuliko kumtunza na kumbakiza
mteja uliyekuwa nawe tangia muda mrefu.
Hivyo kampuni za bima nchini zinatakiwa
kujiwekea malengo na mikakati mbalimbali ili kuleta ufanisi na tija katika
shughuli za ulipaji wa madai mbalimbali ya wateja wao.
Hivyo ni muhimu kwa kila
kampuni ya bima kujiwekea malengo na mikakati mbalimbali ili kuleta tija na
ufanisi katika shughuli za ulipaji madai. Na ili waweze kulibainisha hili, kwa kila kampuni ya bima ni
muhimu kujiwekea mapatano ya utoaji wa huduma baina yake na mteja kwa kuanzisha
mkataba wa huduma kwa wateja.
Mikataba kama hii ya mapatano
itakuwa ni hatua muhimu sana katika utoaji wa huduma bora katika misingi ya
uwazi na uwajibikaji.
Kwa kufanya hivyo wateja wa
kampuni za bima watapata uhuru na uelewa wa kufahamu matarajio yake katika
huduma fulani na hasa viwango vya muda ambavyo vitamwezesha mteja kupanga mambo
yake vyema badala ya kusubiri huduma bila kufahamu upatikaji wa huduma hizo na
kwa viwango vipi.
Kwa mfano kutokana na meneja
mkuu wa bima ya maisha wa Sanlam bwana Wilson Mnzava anasema kama Sanlam wao tayari
wamesha jiwekea mapatano ya utoaji wa huduma baina yao na mteja kwa kuanzisha
mkataba wa huduma kwa wateja.
Anasema mapatano haya
yanamwezesha mteja wao kufahamu huduma za Sanlam, viwango vya huduma na hatua
atakazoweza kuzichukua iwapo viwango vya huduma vitakuwa kinyume na matarajio
ya mkataba.
“Hata hivyo, ili Sanlam iweze
kutoa huduma bora kwa wakati kama ilivyokusudiwa katika mapatano haya,
tunategemea zaidi kupata mwitikio na ushirikiano kutoka kwa wateja ili kutimiza
makubaliana haya. Mteja ndiyo kiungo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa
malengo ya kila siku ya kampuni yetu ya Sanlam, kwa kuwa taarifa anazotoa ndizo
zinazowezesha Sanlam kama kampuni ya bima kutoa huduma stahiki” Wilson Mnzava anasema.
Mnzava anasema wana imani ya
kwamba, kila mteja atatimiza wajibu wake ipasavyo ili aweze kupata huduma bora
zinazotolewa kwa wakati muafaka, kwa heshima na kwa unyenyekevu. Hivyo, maoni
ya mteja yatawezesha Sanlam kuongeza ubora wa huduma unazozitoa.
Bima
ni mfumo wa kumwahidi kumrejeshea mwanachama hali ya afya, kipato, maisha na
ustawi pindi anapopata janga au anapopoteza kitu chake cha thamani hasa ikiwa
amelipia michango ya marejesho yaani premiums.
Bima
hulenga kumkinga mwanachama dhidi ya janga lisilotegemewa, kwa mfano kinga
dhidi ya ajali, mazishi, kulazwa hospitalini, moto, mafuriko, wizi, nk. Aghalabu,
matukio hayo yasipokingwa, hurudisha nyuma maendeleo ya mtu au familia nzima
kiuchumi.
Kutokana na taarifa za robo
mwaka zilizotolewa na msimamizi na
mwangalizi wa bima nchini yaani TIRA kwa Septemba 2016, inaonesha kampuni ya
bima ya Sanlam inaongoza nchini kwa soko la bima ya maisha kwa asilimia 72 ikiwemo na bima ya
mazishi. Taarifa hiyo pia inasema kampuni hii ya Sanlam ipo kwenye soko hili la
bima zaidi ya miaka 100, na ina matawi yake zaidi ya nchi 33 duniani yakiwemo
kwa bara la Afrika, Amerika, Asia, Ulaya na Australia.
No comments :
Post a Comment