NA K-VIS BLOG
WAZIRI Mkuu
mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim amelazwa hospitali jijini Dar es Salaam na leo
Januari 2, 2019, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli, wamemtembelea kumjulia hali na
kumuombea dua.
Picha
za Ikulu
zimemuonyesha Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth, pamoja na familia ya
Dkt. Salim na wasaidizi wa Rais wakimuombea dua pembezoni mwa kitanda
alikolazwa Waziri Mkuu
huyo mstaafu ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi huru
za
Kiafrika (OAU), kwa sasa AU.
Rais Magufuli.
Picha hizo ukiwemo ukanda wa video zinamuonyesha
Rais Magufuli akimsalimia Dkt, Salim na kumuuliza hali hali yake na
kumpa pole. “Niliambiwa jana kuwa hali haikuwa nzuri,
nikawaambia jamani mumsaidie mzee wangu apone.” Alisema kabla ya
kuungana na
mkewe pamoja na familia ya Dk. Salim kumuombea dua ili apone haraka.
Rais Magufuli alisema alijulishwa juu ya ugonjwa unaomsumbua na
amefanyiwa upasuaji baada ya kufikishwa hospitalini hapo jijini Dar es
Salaam. Rais Magufuli pia anauguliwa na mama yake mzazi Bibi
Suzana Magufuli anaesumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi ambapo amekuwa akipatiwa
matibabu kwa takribani miezi mitatu sasa.
Rais
wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiungana na mkewe Mama
Janeth Magufuli, (wapili kushoto mstari wa mbele), Mama Amne Salim
Ahmed Salim, (wakwanza kushoto) ambaye ni mke wa Dkt. Salim, kumuombea
dua Waziri
Mkuu huyo mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim kutokana na maradhi
yanayomsumbua leo
Januari 2, 2019.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu
Mstaafu Dkt.Salim Ahmed Salim hospitalini Jijini Dar es Salaam, alipomtembelea
pamoja na Mkewe Janeth Magufuli ili kumjulia hali.Januari 2 ,2019
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu
Mstaafu Dkt.Salim Ahmed Salim hospitalini Jijini Dar es Salaam, alipomtembelea
pamoja na Mkewe Janeth Magufuli ili kumjulia hali.Januari 2 ,2019
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu
Mstaafu Dkt.Salim Ahmed Salim hospitalini Jijini Dar es Salaam, alipomtembelea
pamoja na Mkewe Janeth Magufuli ili kumjulia hali.Januari 2 ,2019
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiungana na mkewe Mama Janeth
Magufuli, familia ya Dkt. Salim ikiongozwa na mkewe mama Amne Salim Ahmed Salim,
kumuombea dua Waziri Mkuu huyo mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim kutokana na
maradhi yanayomsumbua leo Januari 2, 2019.(PICHA NA IKULU).
No comments :
Post a Comment