Sunday, December 2, 2018

WATOTO 80 WENYE MATATIZO YA MOYO KUFANYIWA UPASUAJI KATIKA KAMBI MAALUM YA JKCI KWA USHIRIKIANO NA LITTLE HEART YA SAUDI ARABIA

Watoto ambao ni wagonjwa wa moyo kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania wakiwa na wazazi wao wakisubiri kulazwa wodini kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa moyo na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana wenzao wa mradi wa afya wa Little Hearts wa nchini Saudi Arabia ambao ni moja ya mradi wa Afya ulioko ndani ya Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao  Makuu yake mjini London nchini Uingereza. Jumla ya watoto 80 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya matibabu ya siku nane.


NA GENOFEVA MATEMU – JKCI

JUMLA ya watoto 80 wenye matatizo ya moyo wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya matibabu itakayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mradi wa Little Heart wa nchini Saud Arabia ambao ni moja ya mradi wa Afya ulioko ndani ya Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao Makuu yake mjini Londoni nchini Uingereza. Matibabu hayo yatahusisha upasuaji wa moyo wa kufungua kifua kwa watoto wenye matatizo makubwa na upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo kwenye paja kwa watoto wenye matatizo yasiyohitaji upasuaji wa kufungua kifua. Watoto wanaotarajiwa kufanyiwa matibabu hayo katika kambi hiyo wameshafika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kufanyiwa uchunguzi wa awali tayari kwa kulazwa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji huo. Kambi hiyo ya siku nane inatarajia kuanza kesho tarehe 1 Desemba 2018 hadi tarehe 8 Desemba 2018 kwa kutoa matibabu ya kina kwa watoto wote walioandaliwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya magonjwa ya moyo. Tangu mwaka 2015  jumla ya watoto 296 wameshafanyiwa upasuaji na madaktari kutoka mradi wa Little Heart kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa JKCI ambapo watoto 111 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na watoto 185 walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua. Hii ni mara ya nne kwa madaktari wa Little Heart wa nchini Saud Arabia ambao ni moja ya mradi wa Afya ulioko ndani ya Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao Makuu yake mjini London nchini Uingereza kuja hapa nchini kwa ajili ya kutoa matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto kwa kushirikiana na madaktari wa JKCI.

No comments :

Post a Comment