Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji akimkabidhi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere tuzo ya uandaaji wa vitabu vya hesabu kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu katika Taasisi za Serikali zinazotumia Mfumo wa Uhasibu wa IPSAS ambapo TRA imeibuka mshindi wa jumla. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) jijini Dar es Salaam mwishoni wa wiki.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (wa tatu kulia) akiwa ameshikilia tuzo ya uandaaji wa vitabu vya hesabu kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu katika Taasisi za Serikali zinazotumia Mfumo wa Uhasibu wa IPSAS ambapo TRA imeibuka mshindi wa jumla. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha cha Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) jijini Dar es Salaam mwishoni wa wiki.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (wa tatu kulia) akiangalia kwa makini tuzo ya uandaaji wa vitabu vya hesabu kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu katika Taasisi za Serikali zinazotumia Mfumo wa Uhasibu wa IPSAS ambapo TRA imeibuka mshindi wa jumla. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha cha Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) jijini Dar es Salaam mwishoni wa wiki.
………………..
Na Veronica Kazimoto
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imeibuka mshindi wa jumla katika tuzo za
uandaaji wa
hesabu bora mwaka 2017 zinazotolewa kila mwaka na Bodi ya
Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).
Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere,
amewaasa wahasibu nchini kuwasaidia wateja wao kuandaa vitabu vya
mahesabu kwa kufuata viwango vya kimataifa ili kuepuka kufanya
marekebisho ya vitabu hivyo na kupotea kwa kodi.
Amesema
taasisi nyingi zimekuwa hazijui kuandaa vitabu vya mahesabu na wakati
mwingine hulipua katika kuviandaa ambapo matokeo yake vimekuwa
vikikataliwa na kutakiwa kurudia mahesabu hayo hali ambayo inafanya kazi
hiyo kuwa ngumu na wakati mwingine inaleta mashaka.
Kichere
amesema siri ya ushindi wao ni ushirikiano mzuri walionao kama mamlaka
ikiwa ni pamoja na kutoa muda wa ziada wa kazi ili kuweza kukidhi
viwango vya kimataifa na kama taasisi ya kukusanya mapato lazima ifanye
hivyo.
“Tumefurahi
kupata tuzo hii inayoonyesha kuwa, tunatengeneza mahesabu yetu kwa
kufuata taratibu na viwango vya kitaifa katika uandaji wa vitabu
vinavyohusiana na fedha. Tumekuwa na ushirikiano mzuri na wahasibu wetu
ambao mara zote wamejitolea muda wao ili kukidhi vigezo hivi vya
kimataifa,” amesema Kichere.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika utoaji wa tuzo hizo, aliwaambia wahasibu kuwa, imani yake ni
kwamba, siku tatu walizokutana wamezitumia vizuri kwa kujadili masuala
mbalimbali yanayowahusu kwa undani.
No comments :
Post a Comment