Kampuni
ya TBL Group, imeadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani kwa wafanyakazi wake
kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Moshi na Arusha, kushiriki
zoezi la upimaji wa afya zao,kufanya mazoezi na kutoa misaada kwa vituo
vinavyolea watoto yatima.
Afisa
Mahusiano ya wafanyakazi wa TBL Group,Salma Nyangasa,alisema
maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yamekuwa yakiadhimishwa na kampuni
kila mwaka kwa kuwashirikisha wafanyakazi wake kupima afya zao “Suala
la afya za wafanyakazi ni jambo ambalo kampuni inalipa umuhimu mkubwa
ndio maana tumetumia siku hii kupima afya sambamba na kushiriki kufanya
mazoezi ya kujenga mwili na kupatiwa semina za kukabiliana na magonjwa
mbalimbali”alisisitiza.

Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakiwasha mshumaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakishiriki mazoezi wakati wa siku ya kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani.
Baadhi
ya wafanyakazi wa kitengo cha TEHAMA (IT) wa TBL, wakikabidhi msaada
kwa Mkuu wa kituo cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu
cha Msimbazi Centre,Sister Stela, ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Ukimwi
Duniani.
No comments :
Post a Comment