Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Maji
Profesa Makame Mbarawa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa
Maji safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha. Wengine katika
picha ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi
na Mawasiliano Isaack Kamwelwe pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi
wa mradi mkubwa wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira utakaosaidia jiji la
Arusha katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Kimyaki Arumeru
mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia maji yanayotoka katika moja
ya visima virefu vilivyopo katika mradi huo mkubwa wa maji safi na
usafi wa mazingira katika jiji la Arusha. Mradi huo utakapokamilika
utaweza kuzalisha lita za ujazo milioni 200 kwa siku tofauti na sasa
ambapo lita za ujazo ni 45 milioni wakati mahitaji ya jiji la Arusha ni
lita za ujazo milioni 90.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru wakati wa mkutano na
wananchi wa Arumeru jijini Arusha mara baada ya kuzindua mradi huo wa
maji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Arumeru
mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Maji safi na usafi wa
Mazingira katika jiji la Arusha
Wananchi wa Arumeru wakishangilia
wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli katika kijiji cha Kimnyaki Arumeru.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati akiondoka katika eneo la mkutano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Meya wa jiji la Arusha
Calist Lazaro mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Arumeru. PICHA NA
IKULU
No comments :
Post a Comment