Sunday, December 2, 2018

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI PAMOJA NA RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA WAFUNGUA KITUO CHA KUTOA HUDUMA KWA PAMOJA MPAKANI NAMANGA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wanachi wa Kenya na Tanzania katika eneo la Mpakani Namanga mara baada ya hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania na Kenya.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wa kupiga picha za pamoja mara baada ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania na Kenya.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akihutubia wanachi wa Kenya na Tanzania katika eneo la Mpakani  Namanga mara baada ya hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania na Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Oldonyo Sambu Wilayani Arumeru wakati akitokea Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya. PICHA NA IKULU



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na   Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipungia wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano pembezoni mwa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi funguo Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea funguo kutoka kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na watoto wawili kutoka Kenya waliofika kumpokea katika kituo cha kutoa huduma kwa pamoja kwa upande wa Kenya.

 Baadhi ya Wananchi wa Kenya na Tanzania waliohudhuria katika hafla ya ufunguzi wa vituo hivyo Mpakani Namanga.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na   Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakielekea upande wa mpaka wa Tanzania mara baada ya ufunguzi wa kituo cha kutoa huduma kwa pamoja kwa upande wa Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na   Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakielekea kupanda gari moja kutoka Arusha mjini kuelekea Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya. (PICHA NA IKULU)
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema kituo kipya cha ukaguzi Namanga kinatarajia kuingizia Tanzania Shilingi Bil. 58 mwaka huu wa fedha, 2018/2019.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Namanga, Jijini  Arusha wakati wa ufunguzi wa kituo hicho uliofanyika mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Rais Magufuli amesema, kukamilika kwa kituo hicho kumeongeza mapato kutoka wastani wa shilingi Bil. 3 kwa mwezi hadi shilingi Bil. 4.5 kwa mwezi ambapo kwa mwaka huu wa fedha Serikali ya Tanzania inatarajia kukusanya jumla ya shilingi Bil. 58 kutoka katika kituo hicho.
 "Ujenzi wa vituo vya huduma za pamoja mipakani vimerahisha huduma za usafiri na kupunguza gharama za muda.Zamani watu walikuwa wakitumia siku nzima kuvuka mpaka, lakini sasa hivi mtu anatumia dakika 15 tu kuvuka mpaka huo," amesema Rais Magufuli.
 Amesema, kituo hicho kitawawezesha wafanyabiashara kuvusha bidhaa zao zaidi ya mara  Kumi kwa mwezi tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo ilikuwa nadra kwa mfanyabiashara kuvuka mpaka huo hata mara Nne kwa mwezi.
 Aidha amesema, kituo hicho kitaimarisha shughuli za biashara na utalii kwa nchi zote mbili kutokana na kurahisishwa kwa huduma ya usafiri pamoja na miundombinu mingine katika kituo hicho.
 Kwa upande wake, Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta amesema ni jukumu lao viongozi kuhakikisha wananchi wanafanyabiashara bila kupingwa na waweze kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili.
 Amesema dhumuni la ujenzi wa kituo hicho ni kuwarahisishia wafanyabiashara wadogo na wakubwa kufanya biashara zao kwa urahisi, ili kila mwana jumuiya wa Afrika Mashariki aweze kunufaika na umoja huo.
 Aidha amewataka wale wote waliopewa jukumu la kusimamia kituo hicho basi wajue kazi yao sio kumnyanyasa mwananchi bali kumsaidia mwananchi afanye biashara yake. Pia wananchi wajue kuwa wakisaidiwa kufanya biashara hawajaambiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya, kuua wanyama au biashara ya magendo bali wanatakiwa kufanya biashara ya haki ili mtu apate fedha yake ya haki.
 Nae, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe Balozi Dkt. Augustine Mahige amesema, kuwa na kituo kimoja cha forodha na uhamiaji kinaboresha soko la pamoja la Afrika Mashariki.
 Vile vile amesema, baada ya soko la pamoja, Jumuiya ya Afrika Mashariki inajiandaa kuwa na sarafu moja ifikapo 2020.
 Kituo cha pamoja Namanga kimejengwa kwa ufadhili wa nchi ya Japani kupitia Shirika la Maendeleo la JICA ambapo kwa upande wa Tazania jumla ya shilingi Bil. 18.6 zimegharamiwa . Aidha Benki ya Maendeleo ya Afrika imefadhili kiasi cha Dola za Marekani 117,000 kwa ajili ya kuweka vifaa vya ofisi kwa upande wa Tanzania na Kenya.

No comments :

Post a Comment