Mwenyekiti
wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Bi.
Mariam Mwaffisi akisoma hotuba yake wakati wa mahafali ya 12 ya chuo
hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu
Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu
ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS,
Profesa Andrea Pembe. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS) Profesa Andrea Pembe akisoma hotuba yake wakati wa mahafali ya
12 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni
Mkuu wa Chuo hicho Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi
na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili Bi. Mariam Mwaffisi.
Kaimu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
Prof. Appolinary Kamuhabwa akiwakaribisha wakufunzi kusoma majina ya
wahitimu.
Mkuu
wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu
wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akimtunuku Shahada ya Uzamili,
mmoja wa wahitimu katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahitimu waliotunukiwa astashahada, stashahada, shahada za
awali na shahada za uzamili wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es salaam.
Bendi ya Jeshi ikisherehesha katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akimtunuku
astashahada, stashahada, shahada za awali na shahada za uzamili wa Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wakati wa
mahafali ya 12 yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
Wahitimu
wa astashahada, stashahada, shahada za awali na shahada za uzamili
katika upande wa afya wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (MUHAS) wakila kiapo cha uaminifu wakati wa mahafali ya 12
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wakifurahia.
Meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa kuhitimisha sherehe.
Meza kuu ikipata picha na baadhi ya wahitimu.
No comments :
Post a Comment