Mkurugenzi wa Idara ya Sera na
Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Ujenzi), Bi. Elizabeth Tagora, akifungua mkutano wa wadau wa Sekta ya
Ujenzi kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya Baraza la Taifa
la Ujenzi (NCC) ili kuimarisha na kuhuisha baraza hilo. Mkutano huo
umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere
(JNICC), jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa
la Ujenzi (NCC), Dkt. Matiko Mturi, akizungumza na wadau mbalimbali wa
Sekta ya Ujenzi (hawapo pichani), waliohudhuria mkutano wa kujadili
mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya baraza hilo, jijini Dar es
Salaam.
Wadau mbalimbali kutoka Sekta za
Ujenzi hapa nchini waliohudhuria mkutano wa kujadili mapendekezo ya
marekebisho ya sheria ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), wakimsikiliza
Mtendaji Mkuu wa baraza hilo Dkt. Matiko Mturi (hayupo pichani), katika
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius
Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya wadau wa sekta
ya ujenzi waliokutana kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya
Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), ili kuimarisha na kuhuisha baraza hilo.
No comments :
Post a Comment