HakiPensheni
Na Christian Gaya
www.majira.co,tz
Ijumaa 09 November 2018
Haki
ya taarifa kwa mwanachama kwa wakati huu wa mabadiliko ni ya muhimu sana,
ukichukulia asili ya ugumu wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii na juu ya ugumu
wa uelewa wa elimu ya fedha na pensheni kwa wanachama na kwa wananchi kwa
ujumla.
Kama
miaka kadhaa tumetoka kwenye mfumo rahisi wa hifadhi ya jamii wa kuweka akiba
ambapo hali hatarishi zote za mfuko wa akiba huachiwa mwanachama pekee na
kuingia ...
kwenye mfumo mgumu zaidi wa mpango wa pensheni ya hifadhi ya jamii
unaondeshwa kwa mfumo wa bima ambapo mwanachama anaahidiwa mafao yote kwa
mkataba maalumu atakayopatiwa kuanzia mwanzo anapojiunga yakiwepo ya muda mfupi
na ya muda mrefu.
Mwanachama
kupata taarifa na kummilikisha kwa njia ya kumhamisisha na kumwezesha awe uwezo
wa kufanya maamuzi. Mara nyingi mwanachama anapatiwa habari na kujua
kinachoendelea inakuwa ni magurudumu mazuri zaidi ya kuongeza mwendo wa uwazi
na uwajibikaji wa uongozi wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii.
Ikumbukwe
ya kuwa mifuko ya pensheni huudwa chini ya bodi ya wadhamini wanaokuwa na
wajibu wa kusimamia wanaosimamia mfuko. Haki ya kupata habari kwa upande mmoja
ina maana ni haki ya wanachama kujua mfuko wao wa pensheni na kwa upande
mwingine ni wajibu wa bodi ya wadhamini kutoa habari kwa wanachama wa mfuko
Kila
mfuko unasimamiwa kablasha ya sheria linaloeleza wazi taratibu, vigezo na
masharti ya mfuko. Katiba hii kumbukumbu ya habari na taarifa zote zinazohusu
mfuko. Ni jambo la muhimu ya kuhakikisha ya kuwa mwanachama wanajizoesha
wenyewe na sheria za mfuko wao na hata kuziweka na kuziandika kwenye vijitabu
vidogo ambayo vimefupisha habari zote za
msingi zinazohusu mfuko.
Kijitabu
kidogo kinalenga kuwa na maelezo yote muhimu kwa lugha ya wazi na rahisi
kusomeka bila kwenda nje ya katiba ya mfuko. Bila ya kuzingatia mfuko uko
mazingira gani inapotoa mpango wa pensheni kwa wanachama, haki ya kupata habari
ziko katika njia nne zifuatazo.
Taarifa
za Msingi za Mfuko
Wanachama
wanatakiwa wawe na uwezo wa kujibu maswali ya msingi yanayohusu mfuko wao, kama
vile: ni akina nani wadhamini wa mfuko? Ni nani anastahili kuwa mwanachama wa
mfuko? Ni jinsi gani wanachama wanaunda mafao? Je wanachama wanachangia kwenye
mfuko? Ni kiasi gani wanachama wanachangia? Je mwajiri anachangia? Ni kiasi
gani mwajiri anachangia? Ni umri wa miaka mingapi wanachama wanatakiwa kustaafu
kwa hiyari au mapema Ni baada ya miaka mingapi wanachama wanastahili kustaafu
kwa lazima? Ni mafao ya gani wanachama wa nastahili kupata kabla na baada ya
kustaafu kazini?
Taarifa
hizi zote zinaweza kupatikana kwenye katiba, kajitabu cha mwanachama (kama
kipo) au kwa kuuliza idara ya mawasiliano, masoko na huduma kwa wateja au ofisi
yeyote zilizotapakaa karibu nchi nzima
Makablasha
ya Kisheria.
Pamoja
na katiba ya sheria, wanachama wana haki ya kukagua mahesabu ya mfuko
yaliyokaguliwa kisheria na mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali. Mwanachama
vile vile ana haki ya kukagua nyaraka kama vile marejista yote yanayoyotunza kumbukumbu
za mfuko pamoja na taarifa za uwekezaji
Kumbuka
ya kuwa, mfuko umeanzishwa kwa ajili ya kumnufaisha mwanachama wake na kazi
kubwa ya wadhamini ni kulinda maslahi ya mwanachama kwenye mfuko
Mkutano mkuu wa Mwaka wa Wanadau na
Wanachama
Mifuko
yote inatakiwa kufanya mkutano mkuu wa wanachama na wadau ambapo wanachama
wanaalikwa kuhudhuria. Wanachama wanaohudhuria wanapata taarifa zote na matukio
mbalimbali kutoka kwa wadhamini wa mfuko na kwa watoa huduma ambao ni viongozi
wa mfuko, wakaguzi wa mahesabu, wataalamu na mameneja wa mfuko pamoja na
wawakilishi wa umoja wa vyama vya wafanyakazi makazini, na wawakilishi wa
serikali. Mkutano mkuu unatoa fursa kwa wanachama kuuliza maswali kwa wadhamini
na watoa huduma juu ya kila kitu kinachohusu mfuko.
Pamoja
na kupata matukio yote yanayohusu utendaji na maendeleo ya mfuko, mkutano mkuu
hutoa nafasi kwa wanachama juu ya mabadiliko yoyote yanayohusu mafao ndani ya
mfuko na jinsi mafao yao yatakavyoleta mabadiliko yeyote. Kwa kweli badiliko
lolote juu ya mafao yanatolewa na mfuko lazima yataambatana na mabadiliko ya
sheria na vigezo pamoja na masharti yake.
Taarifa za Mahesabu ya wanachama
Wanachama
wanastahili kupewa taarifa zao kila mwisho wa mwaka wa fedha. Hizi taarifa za
hutoa taarifa juu ya mafao mwanachama anayostahili kila mwisho wa mwaka
unaofanyiwa mabadiliko
Kwa mwanachama wa mfuko wa
akiba ya wafanyakazi, taarifa hutoa maelezo juu ya michango iliyochangiwa na
mwanachama na mwajiri wake, na riba iliyopitishwa na wadhamini kwa mwisho wa
mwaka na idadi ya michango yote ya mwanachama pamoja na riba ya mwisho wa
mwaka. Na kwa wanachama wa mfuko wa pensheni unaondeshwa kwa mfumo wa bima.
Mfuko wa pensheni unaoshughulika
na wafanyakazi wa sekta binafsi yaani NSSF, na mfuko wa pensheni wa kwa ajili
ya watumishi wa umma (PSSSF) hupewa maelezo juu ya aina za mafao ambayo
mwanachama anastahili kupatiwa na mfuko kama vile mafao ya muda mrefu na ya
muda mfupi ambapo yote huendeshwa kwa mfumo wa bima.
Haki
ya kupatiwa taarifa inahamasisha uwazi, ufahamu na uelewa na uwajibikaji wa
mifuko ya hifadhi ya jamii. Pia inamwandaa mwanacham kupata fursa ya
kuhakikisha na kulinganisha taarifa ili kulinganisha na kufananisha na ukweli
na michango yao Pamoja na kuwa na haki
ya kupata taarifa, wanachama pia lazima wajue juu ya haki za mafao na haki zao
zingine kwa ujumla.
Taarifa za Mahesabu ya wanachama
Wanachama
wanastahili kupewa taarifa zao kila mwisho wa mwaka wa fedha. Hizi taarifa za
hutoa taarifa juu ya mafao mwanachama anayostahili kila mwisho wa mwaka
unaofanyiwa mabadiliko
Kwa mwanachama wa mfuko wa
akiba ya wafanyakazi, taarifa hutoa maelezo juu ya michango iliyochangiwa na
mwanachama na mwajiri wake, na riba iliyopitishwa na wadhamini kwa mwisho wa
mwaka na idadi ya michango yote ya mwanachama pamoja na riba ya mwisho wa
mwaka. Na kwa wanachama wa mfuko wa pensheni unaondeshwa kwa mfumo wa bima
Mfuko wa pensheni
unaoshughulika na wafanyakazi wa sekta binafsi yaani NSSF, na mfuko wa pensheni
wa kwa ajili ya watumishi wa umma (PSSSF) hupewa maelezo juu ya aina za mafao
ambayo mwanachama anastahili kupatiwa na mfuko kama vile mafao ya muda mrefu na
ya muda mfupi ambapo yote huendeshwa kwa mfumo wa bima.
(Inaendelea wiki ijayo)
No comments :
Post a Comment