Friday, November 30, 2018

SIKU YA UKIMWI DUNIANI:UNAIDS KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPAMBANA NA UKIMWI


Balozi wa Vijana ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Balozi wa Vijana ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo akizungumza na hadhira ya vijana (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Pichani ni Hawa Musa (20) mmoja kati ya vijana zaidi ya 2000 wanaonufaika na mafunzo ya ujasiriamali yaliyofadhiliwa na Shirika la EGPAF ambapo mafunzo hayo yamewasiaida kutengeneza bidhaa mbalimbali  ikiwemo vikoi, mikoba ya shanga, Ubuyu, sabuni za maji na miche ambazo zinawasaidia kupata fedha za matumizi mbalimbali akishiriki kuonyesha kazi zake katika mabanda ya kijiji cha Vijana wakati wa hafla ya kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi yanayofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Bi .Mwanahamisi Mukunda akizungumza jambo kwa niaba ya Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge wakati akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Bi .Mwanahamisi Mukunda aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko wakipata maelezo kutoka kwa Bi. Debora Frank (kushoto) ambaye ni Afisa Miradi wa Huduma za Vijana  wa shirika la EGPAF ambao wanaotekeleza mradi wa USAID wa Boresha Afya kwa kushirikiana na ENGENDER Health kuimarisha afya za watanzania wote na kuongeza upatikanaji wa huduma za afya timilifu za kiwango cha juu na jumuishi wakati alipotembelea kijiji cha Vijana kwenye hafla ya kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi yanayofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma. Mradi unaolenga kuboresha huduma za kinga na matibabu ya VVU/UKIMWI, uzazi wa mpango, Kifua Kikuu na kutoa huduma mahususi wa kuyafikia makundi  maalum kwa watoto na vijana.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko,  Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Bi .Mwanahamisi Mukunda pamoja na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng wakipata maelezo kutoka kwa Mshauri mwandamizi wa masuala ya afya ya uzazi kwa vijana kutoka mradi wa Sauti unaratibiwa na Shirika la JHPIEGO, Esther Majani (wa kwanza kushoto) kuhusu shughuli wanazofanya za kutoa elimu ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa makundi hatarishi ikiwemo mabinti walio nje ya shule wa miaka 15-24 wakati walipotembelea kijiji cha Vijana kwenye hafla ya kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi yaliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa kiufundi-FP wa shirika la JHPIEGO, Bi. Lena Mfalila (kushoto) kuhusu shughuli zinazoendeshwa na Shirika hilo kupitia mradi wa Tupange Pamoja (TCI)  ambayo ni huduma rafiki ya vijana katika afya ya uzazi kwa vijana wakati walipotembelea kijiji cha Vijana kwenye hafla ya kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi yayonafanyika Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Mtaalamu wa kiufundi-AYSRH wa shirika la JHPIEGO kupitia mradi wa Tupange Pamoja (TCI), Bw. Waziri Njau (katikati) pamoja na ‘Coacher’ -SRH wa shirika la JHPIEGO kupitia mradi wa Tupange Pamoja (TCI),Bi Rehema Mzungu.


Msanii wa Bongo Flava Maua Sama akitoa burudani kwa wakazi wa Dodoma wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde (wa pili kushoto) akiwasili kwenye viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Bi .Mwanahamisi Mukunda (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng (kulia) wakielekea kutembelea kijiji cha Vijana wakati wa hafla ya kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi yayonafanyika Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akihutubia wananchi wa Dodoma wakiwemo vijana wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Pichani ni baadhi ya kazi za mshindi wa kwanza katika eneo la uchoraji Edward Malongo (tisheti nyeupe)  wa picha zinatoa ujumbe wa kuhamasisha kampeni ya kutokomeza VVU zikionyeshwa kwa wageni wa meza kuu wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Kutoka kushoto kwenda kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Madawa ya Kulevya na Ukimwi ambaye pia ni Mbunge wa Biharamulo, Mhe. Oscar Mukasa, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Bi .Mwanahamisi Mukunda, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng pamoja na Balozi wa Vijana ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Madawa ya Kulevya na Ukimwi ambaye pia ni Mbunge wa Biharamulo, Mhe. Oscar Mukasa akitoa salamu za kamati yake wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akikabidhi zawadi ya kombe ya mshindi wa kwanza kwa kapteni wa timu ya mpira ya vijana walio nje ya shule ya Panama, Bw. Dunia Salumu wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Afisa Maendeleo Vijana wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Tumsifu Mwasambale (kushoto) akionyesha moja ya picha iliyoshinda wakati wa wiki ya shughuli za kijiji cha vijana iliyochorwa kijana Edward Malongo na kupigwa mnada ambapo zaidi shilingi 2.7 zilipatikana ambapo nusu zilienda kwa mchoraji na nyingine kwenye mfuko wa udhibiti wa Ukimwi (ATF) wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Uzazi Salama mkoa wa Dodoma wa Shirika la PSI Tazania, Bi. Sophia Jamal (kushoto) kuhusu elimu ya afya ya uzazi wanayotoa kwa mabinti kuanzia miaka 13-19 yenye kauli mbiu ya Binti “Dhamiria kutimiza ndoto yako-“Simama Imara” “Vaa Taji”, “Kua Mzuri” wakati alipotembelea kijiji cha Vijana kwenye hafla ya kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi yanayofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Mchekeshaji maarufu nchini Stan Bakora akitoa burudani ya kuhamasisha upimaji wa UKIMWI kwa njia ya vichekesho wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akipata maelezo kutoka kwa Meneja masoko wa Shirika lisilo la kiserikali la T-MARC Tanzania, Bi. Sophia Komba kuhusu shirika hilo linalotoa elimu kuhusu matumizi ya Kondomu ili kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya ngono ikiwa pamoja na UKIMWI katika mabanda ya kijiji cha Vijana wakati wa hafla ya kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma. T-MARC Tanzania wanafanya kazi kwa kushirkiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto katika kuboresha afya ya jamii ya watanzania ambapo pia ni wasambazaji wa bidhaa za afya ambazo ni Kondomu ya kiume- Dume, Kondomu ya kike Lady Pepeta na vidonge vya uzazi wa mpango-Flexi P. Wa pili kushoto ni Outreach Educator wa T-MARC Tanzania, Dotto Iddy.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akitoa neno kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akikabidhi zawadi ya kombe ya mshindi wa kwanza kwa kapteni wa timu ya mpira wa pete ya Vijana Queens, Ngesa Selemani wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Pichani juu na chini ni sehemu ya wakazi wa Dodoma walioshiriki hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Pichani juu na chini ni sehemu ya wakazi wa Dodoma walioshiriki hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.


Pichani juu na chini ni sehemu ya wakazi wa Dodoma walioshiriki hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng amesema kuwa kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya Ugonjwa huo. Akizungumza jana Jijini Dodoma wakati wa kilele cha shughuli za vijana kuelekea maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, Dk Zekeng alisema kwamba kuna haja kubwa ya kuhakikisha kwamba taifa linapambana na maambukizi mapya kwa kuhakikisha kwamba kunatolewa huduma rafiki miongoni mwa vijana ambao ndio kundi kubwa linalohitaji msaada kwa sasa ni jukumu la kila mwanajamii na kuomba ushirikiano wadau wote katika mapambano hayo. Alisema wakati taifa nusu yake ni vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 na huku takwimu zikionesha kwamba kundi hilo linaathirika sana ipo kila sababu ya kutengeneza mkakati na kuweka mazingira rafiki ili kuokoa kizazi hicho. Alisema kwa sasa vijana wanahitaji kusaidiwa kwa kuwaweka katika mazingira rafiki ya kuhitaji huduma zinazotolewa katika kampeni ya kukabiliana na maambukzi ya VVU.Alisema kwa sasa huduma hizo si rafiki ziko chache na hivyo kuwafanya vijana wasishiriki kwa sababu ya hofu ya kunyanyapaliwa na pia kukosekana kwa elimu hitajika.Aliongeza ili taifa lifikie uchumi wa kati unaotakiwa mwaka 2025 na kufikia agenda 2030 ni lazima liwe ni taifa lenye vijana wanaojitambua na wenye afya bora.“iko haja ya kushawishi vijana ambao ndio kundi kubwa kujitambua na katika package nzima wajue namna ya kujikinga, na kuishi kwa afya hata kama wana virusi” alisema Dk Zekeng  na kusisitiza kwamba shirika lake litaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha kwamba vijana wanapatiwa elimu ya kutosha na mahitaji mengine katika vita dhidi ya UKIMWI.Alibanisha kuwa takribani watu milioni 37 Duniani wanaishi na Virusi vya UKIMWI na sehemu kubwa wakiwa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.Siku ya UKIMWI Duniani huadhimishwa kila ifikapo Disemba Mosi kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi ambapo mwaka huu yanafanyika Jijini Dodoma na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Warizi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majali

No comments :

Post a Comment